Wednesday, July 23, 2014

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS ,KAZI MAALUM ,PROFESA MARK MWANDYOSA AFANYA ZIARA YA KIKAZI MAKAO MAKUU YA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA

01
. Kaimu Mkurugenzi Mkuu , Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)  Dk.  james Diu( Kulia ) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya  wakati alipotembelea  makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kujionea shughuli zinazofanywa na TCAA.
02
.Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum , Prof Mark Mwandosya akikabidhiwa  Nyaraka ya Sheria  ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA  na  Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka hiyo  Dk. James Diu , wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya ofisi hiyo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa hapo.
03
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu , Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)  Dk.  james Diu( Kushoto)akiagana na   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Prof. Mark Mwandosya mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi  makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kujionea shughuli mbambali zinazofanywa na TCAA. Kulia anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya TCAA, Rubeni Ruhongore.
04
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum , Prof Mark Mwandosya, akisisitiza jambo  kuhusiana na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati alipokutana na Uongozi wa  Mamlaka hiyo  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu , Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)  Dk.  james Diu.
05
.Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya  akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Rubeni Ruhongore wakati alipokuwa akimuelezea shughuli zinazofanywa na TCAA  wakati Waziri huyo alitembelea Makao Mkuu ya Mamlaka hiyo kwa ajili ya ziara ya  kujionea shughuli  zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
-7
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kiusalama wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),  akifafanua wakati wa ziara ya  Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya  Makao Makuu ya TCAA  jijijni Dar es Salaam.
08
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  na Mamlaka zingine za Udhibiti Nchini wakati alipotembelea Makao Makuu ya TCAA, Dar es Salaam.
10
Meneja  Mahusiano wa  Mamlaka ya Udhibiti  Usafiri wa  Nchi Kavu  na Majini –(SUMATRA) David Mziray akifafanua jambo wakati wa ziara ya Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya  TCAA makao makuu

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...