Wednesday, July 16, 2014

MADUKA MATATU IKIWEMO NYUMBA VYATEKETEA KWA MOTO MWANANYAMALA

 Moto ukiwa umeanza kama utani, watu wakiwa wanaendelea na kazi kama kawaida. Moto mkubwa uliosababishwa na hitirafu ya umeme  umewaka eneo la Mwananyamala Jirani na Hospitali ya Mwananyamala na kusababisha kuungua kwa Maduka matatu pamoja na nyumba moja ambayo ilikuwa imeungana na duka moja wapo ambamo walikuwa wanauza vitambaa na kushona nguo.
Moto huo ulichukua zaidi ya masaa mawili ambapo wakazi wa eneo hilo ndio waliosaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto huo mpaka kuumaliza na baadae Kikosi cha kuzima moto kufika na kukuta moto ndio unaishia na kuendelea kumalizia kushirikiana na wananchi wengine kuzima moto huo.

Katika tukio la Moto huo hakuna mtu ambaye amedhurika ingawa katika maduka yote matatu walifanikiwa kuokoa baadhi ya vitu huku vilivyobakia vikiteketea vibaya kwa moto huo.
 Moshi ukiwa unazidi katika eneo ambalo maduka matatu yameteketea kwa moto.
Gari likiwa linarudi nyuma lilipotokea baada ya kuona kuna moshi mkubwa mbele yao.
 Mashuhuda wakiwa wameanza kuelekea eneo la tukio
 Moto ukiwa unaanza kupamba moto, waya wa umeme unao onekana unashuka chini ndio umesababisha moto huo.
 Moto ukiwa unazidi pamba moto katika duka la kushonea nguo na kuuza vitambaa.
 Duka la nguo likiwa linapamba moto na maduka mengine yakiwa yameanza kupamba moto pamoja na nyumba ambayo ilikuwa imeungana na duka.
 Mmoja ya vijana akiwa anaanza kuokoa vitu vyake jirani na maduka yaliyokuwa yakiungua.
 Moto ukiwa unazidi
 Mamia ya watu wakiwa wamefika kushuhudia  tutuki la Moto
 Vijana wakiwa bize wanafanya kazi ya kuendelea kuzima moto kwa ushirikiano
 Vijana wakiwa wanashughulika kwa nguvu zote ili wapate kuzima moto mara moja
 Baadhi ya Mashuhuda wakimwagiwa maji kupisha njia ya waokoaji waliojitolea kuzima moto kupita
 Mmoja wa Mashuhuda akiwa anachukua tukio kwa umakini
 Kikosi cha zima moto wakiwa wakiwa wanawasili eneo la tukio, huku wananchi wakiwazuia wasifanye kazi kwa kuwa kazi wamekuta imeisha
 Kikosi cha zima moto wakiwa wameanza shuguli ya kumalizia kuzima moto
Maji ya kuwasha yakiwa yamefunguliwa ili kuwatawanya watu wakae mbele kupisha kazi ya kuzima moto na uharifu.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...