Mgeni rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akiwaonesha wajumbe wa Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mfumo wa Kushughulikia Malalamiko ulioandaliwa na Ofisi hiyo mara baada ya kuuzindua katika kikao cha kwanza cha Baraza hilo mkoani Tanga. Katikati ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
Mgeni rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akiwaonesha wajumbe wa Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Ofisi hiyo mara baada ya kuuzindua katika kikao cha kwanza cha Baraza hilo mkoani Tanga. Katikati ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akimkabidhi mgeni rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) Mkataba wa Huduma kwa Mteja katika kikao cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika mkoani Tanga. Katikati ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab.
Mgeni rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akimkabidhi cheti kama zawadi ya Mfanyakazi bora Bi. Sylivia Meku ambaye ni Mtakwimu Mkuu na Mwenyekiti mpya wa TUGHE –Tawi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kikao cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika mkoani Tanga. (PICHA ZOTE NA NBS, TANGA)
No comments:
Post a Comment