Tuesday, July 08, 2014

MAWAZIRI WAMIMINIKA NDANI YA BANDA LA METL GROUP MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR

DSC_0086Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akiwasili kwenye banda la Makampuni ya MeTL GROUP na kulakiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji (wa pili kushoto). Kulia ni Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali na Kushoto ni Afisa Mauzo wa MeTL GROUP, Yusuf Sadiq.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
DSC_0063Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid na mkewe akiwasili katika banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0064Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer ( wa pili kulia) akimkaribisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid kwenye banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Kulia ni Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali.
DSC_0090Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Makampuni ya MeTL GROUP linalotoa huduma za bidhaa mbalimbali zikiwemo Soda, Unga, Mafuta ya kupikia, Sabuni za kufulia na Sabuni za kuogea na vingine vingi.
DSC_0070Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Makampuni ya MeTL Group huku Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer akishuhudia tukio hilo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0097Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer (wa pili kulia) akimuelezea mchanganyiko uliotumika kutengenezea Soda zinazozalishwa na kiwanda cha AOne chini ya kampuni ya MeTL GROUP Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) aliyetembelea banda hilo jana kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0100Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer akimwonyesha kinywaji kipya cha “MO Bomba” (Energy Drink)inayozalishwa na Aone kampuni mama ya vimiminika ya MeTL GROUP, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) aliyetembelea banda hilo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0118Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer (katikati) akitoa maelezo ya mali ghafi zinazotumika kutengenezea Mafuta ya kupikia yanayozalishwa na kiwanda cha East Coast Oils and Fats chini ya makampuni ya MeTL GROUP kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) aliyetembelea banda hilo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0124Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akikagua moja ya madumu ya mafuta yanayotengenezwa na kampuni ya MeTL GROUP alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar . Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer.
DSC_0143Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer akimkabidhi zawadi ya Vitenge na Khanga vinavyozalishwa na kiwanda cha 21st CENTURY Textile Ltd chini ya Makampuni ya MeTL GROUP alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0146Mdhibiti ubora idara ya sabuni za kampuni ya MeTL GROUP, Cuthbert Sangiwa Msuya akitoa maelezo ya utengezaji wa sabuni na vipodozi vya kampuni hiyo kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) ( wa tatu kulia) alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer.
DSC_0004Umati wa wakazi wa jiji la Dar wakimiminika kujipatia mahitaji maalum kwenye banda la makampuni ya METL kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar
DSC_0186Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (wa pili kushoto) akimwonyesha bango la kampuni ya mama ya MeTL GROUP, STAR OIL Ltd wauzaji wa mafuta magari Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) aliyembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...