Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam. Jeshi la Magereza linashiriki katika Maonesho ya 38 ya Biashara Mwaka 2014 ambapo Wananchi wanakaribishwa kuja kutembelea Banda la Jeshi la Magereza ili waweze kupata bidhaa mbalimbali za Samani za ndani zenye ubora wa hali ya juu pamoja na bidhaa nyinginezo za ngozi zinazozalishwa na Jeshi la Magereza.Sofa seti iliyotengenezwa kwa Ustadi mkubwa na Mafundi Stadi wa Jeshi la Magereza kama inavyoonekana katika picha. Sofa hiyo imetengenezwa kwa kutumia Mbao aina ya Mkongo ambao ni imara na hudumu kwa muda mrefu zaidi.
Kabati la Vyombo ambalo limetengenezwa kwa Ustadi mkubwa na Wataalam wa Jeshi la Magereza. Kabati hilo la Vyombo limetengenezwa kwa ubao aina ya Mninga.Meza ya chakula yenye viti sita iliyotengenezwa kwa kutumia mbao aina ya Jakaranda inayopatikana katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Iringa. Meza hiyo ya duara imetengenezwa na Mafundi Stadi wa Jeshi la Magereza katika Kiwanda cha Samani cha Arusha ambacho kinamilikiwa na Jeshi la Magereza.Kitanda kilichotengenezwa kwa Ustadi mkubwa na Mafundi wa Jeshi la Magereza. Kitanda hicho kimetengenezwa kwa mbao aina ya Jakaranda inayopatikana katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Iringa.Kiti cha kunesa Maalum kwa ajili ya Watu Wazima kinapatikana katika Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Viwanja vya Maonesho 38 ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment