Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akisalimiana kwa furaha mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi cha FRELIMO cha nchini Msumbiji, Bw. Filipe Nyusi ambaye ametembelea nchini kwa lengo la kutafuta kura kwa wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania kufuatia kampeni za urais zinazoendelea nchini kwake . Waziri Membe alimwandalia chakula cha jioni katika Hoteli ya Hyatt Regency.
Mhe. Filipe Nyusi akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Marcel Escure
Mhe. Nyusi akisalimiana na Mbunge na Mfanyabiashara maarufu nchini, Mhe. Mohammed Dewji.
Waziri Membe akisalimiana na mtoto wa Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Samora Machel, Samora Samora ambaye aliambatana na mgombea huyo wa Urais.
Waziri Membe akimkaribisha Mhe. Filipe Nyusi na Ujumbe wake (hawapo pichani) katika Chakula cha jioni kilichoandaliwa katika Hoteli ya Hyatty Regency Jijini Dar es Salaam
Mhe. Filipe Nyusi akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Membe (hayupo pichani)
No comments:
Post a Comment