Wednesday, March 20, 2013

Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa India Nchini wasaini Mkataba wa Makubaliano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya India

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (kulia) kwa pamoja na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Debnath Shaw wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati ya Chuo cha Diplomasia (CFR) cha Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya India (ICWA). Uwekaji saini huo ulifanyika Wizarani jana tarehe 19 Machi, 2013.
 Bw. Haule akibadilishana Mkataba na Balozi Shaw mara baada ya kusaini.
 Katibu Mkuu, Bw. Haule pamoja na Balozi Shaw wakionesha Mkataba huo.
 Katibu Mkuu Bw. Haule akizungumza na Balozi Shaw mara baada ya kukamilisha zoezi la uwekaji saini mkataba wa Ushirikiano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya India.
 Mhe. Balozi Shaw akichangia hoja wakati wa mazungumzo na Bw. Haule huku wajumbe wengine wakisikiliza.
 Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Mohammed Maundi (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairukiwakishuhudia uwekaji saini wa mkataba huo.
Wajumbe wengine waliohudhuria katika tukio hilo la uwekaji saini wa mkataba. Kutoka kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi wa India hapa nchini, Bw. Gobal Krisha  na Bw. Ali Ubwa, Afisa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha Sheria.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...