Tuesday, March 26, 2013

TAARIFA JUU YA KANUSHO LA WATU WANAOTUMIA JINA LA FLAVIANA MATATA


Tunapenda kuutaarifu umma ya kuwa kuna genge la watu wanaotumia jina la mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata katika mtandao wa kijamii wa Facebook ili kuwarubuni wasichana. Kuna ukurasa ujulikanao kama Flaviana Matata’s hutumika kama moja ya ukurasa wa Mwanamitindo huyu kitu ambacho si kweli. Watu hawa huwarubuni wasichana na kuwaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi kwa mgongo wa Mwanamitindo huyu.  Genge hili la uhalifu hudai kuwa kuna ‘kaka’ yake Flaviana ambaye hukutana na wasichana hawa na baada ya mazungumzo anawalaghai kwa njia mablimbali. Pia wahusika hawa hutoza kiasi cha pesa hata kufikia shilingi laki mbili (200,000 )kama tozo  kwa huduma hii ya kuwatafutia kazi nje ya nchi.
Compass Communications kama kampuni inayosimamia shughuli za Flaviana Matata inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata hahusiki kwa njia yoyote na ukurasa huu au watu hawa.
 Pia tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe waangalifu kwani Flaviana Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia mtu yoyote kazi ya Uanamitindo popote pale.
Ukurasa halisi ya Flaviana Matata kwenye mtandaomwa Facebook ni “Flaviana Lavvy Matata” .
Hivi sasa tunaendelea kushirikiana na vyombo husika kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu huu na tunaomba ushirikiano wenu pia Wanajamii.
Imetolewa na
Compass Communications

No comments:

TUME YA MADINI YAAINISHA MIPANGO YA KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Uanzishwaji wa masoko ya madini wapunguza utoroshwaji wa madini Elimu yatolewa kwa wachimbaji wadogo wa madini CHUNYA Ikiwa ni mkakati wa  k...