Thursday, March 14, 2013

Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar yatembelea NHC

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii (wa tano kutoka kulia), Susan Omari, akiwaelekeza Waheshimiwa wawakilishi namna ujenzi wa mradi wa nyumba wa makazi za gharama nafuu Kibada unavyoendelea. Nyumba hizo zote 218 za awamu ya kwanza zimeuzwa ndani ya saa 48.
Baadhi ya nyumba za mradi wa nyumba wa makazi za gharama nafuu Kibada unavyoendelea. Nyumba hizo zote 218 za awamu ya kwanza zimeuzwa ndani ya saa 48.
Injinia Haikameen Mlekio akiwaelekeza wawakilishi namna mradi huo wa nyumba utakavyokuwa.

Baadhi ya nyumba za mradi wa nyumba wa makazi za gharama nafuu Kibada unavyoendelea. Nyumba hizo zote 218 za awamu ya kwanza zimeuzwa ndani ya saa 48.

 Jengo la Makazi la Mindu lililopo Upanga ambalo ujenzi wake kwa kiasi kikubwa umekamilika. Jengo hilo lina jumla ya sehemu za nyumba 60 na zote zimeshauzwa kwa wahitaji.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imefanya ziara ya siku moja ya kutembelea Shirika la Nyumba la Taifa kujifunza namna ya uendeshaji wake , mafanikio na changamoto wanazopata ili kuweza kujenga welewa mzuri kwaajili ya kuweza kuanzisha Shirika la Nyumba la Zanzibar hivi karibuni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Ofisi za NHC makao Makuu Barabara ya Mandela Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Makame Mshimba Mbarouk alisema kilichowavutia kufika katika Shirika hilo ni sifa za utendaji na namna linavyoendeshwa Shirika hilo.

"Kilichotufikisha hapa leo ni sifa za kiutendaji za vijana hawa za kitanzania ambazo tumekuwa tukizisikia na kwa kuwa nasi tuna Idara ya Nyumba ya Zanziba tunayoazimia kuibadilisha kuwa Shirika, hatuwezi kuanza hovyo hovyo tu, tumeona ni bora tufike tujionee na kujifunza wanavyoendesha Shirika hili,"alisema Mshimba.

Alisema watayafanyia kazi mafunzo waliyoyapata katika ziara yao ya mafunzo na kuyawasilisha katika Baraza la Wakilishi ili kusudi kuweza kufanya maamuzi sahihi. Wawakilishi hao wanaendelea na ziara za mafunzo ambapo kesho watatembelea Shirika la Umeme Tanesco.(Habari na picha zote kwa hisani ya NHC)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...