Balozi
wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram Mukama Biswalo (kulia)
akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto),
baada ya kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Adis
Ababa, akitua kwa muda kwenye Uwanja huo akiwa safarini kwenda China kwa
ziara ya kikazi. Wengine kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM
(Zanzibar), Vuai Ali Vuai na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca
Msambatavangu na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk.
Asha-Rose Migiro na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Titus Kamani.
Msaidizi
wa Katibu Mkuu wa CCM, Edward Mpogolo (kushoto) na Ofisa
anayeshughulikia Siasa za Kimataifa, Makao Makuu ya CCM, Amos Siantemi
wakiratibu taratibu za safari ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana kwenda China, leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere. Maofisa hao pia walikuwa sehemu ya msafara huo.
Mkuu
wa Kitengo cha Itifaki na Uhusiano wa Kimataifa wa Makao Makuu ya CCM,
D. U. H. Mshana na Mkuu wa Kitengo cha Sera za Jamii na Mahusiano ya
Umma, Jasinta Mboneko na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa ya CCM, Juliana Chitinka wauaga ujumbe wa CCM
wakati ukiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliokuwa
ukienda china kwenye ziara ya kikazi ya siku kumi ikiongozwa na Kinana.
Baadhi
ya viongozi na maofisa wa Chama waliopo kwenye msafara huo wakiwa
kwenye basi maalum kwenda kupanda ndege ya Ehiopian Airlines wakati wa
safari hiyo,
Baadhi
ya viuongozi na maofisa wa Chama wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Addis
Ababa baada ya msafara wa Kinana kutua kwa saa sita kwa ajili ya
kuendelea na safari ya kwenda China jioni hii.Picha zote na Bashir
Nkoromo
No comments:
Post a Comment