Rais Kikwete Atembelea Kujionea Mwenyewe Shughuli za Uokoaji Zinavyoendelea Baada ya Jengo la Ghorofa 16 Kudondoka Jijini Dar es Salaam na Kusababisha Vifo vya Watu 20
Eneo la tukio ambapo jengo
la ghorofa zaidi ya 10 liliporomoka jana asubuhi na hadi kufikia saa
sita mchana jana maiti 18 zilikuwa zimeopolewa na watu wanne wakiwemo
wakandarasi waliokuwa wanajenga pamoja na wahandisi wa halmashauri ya
wilaya ya Ilala wanashikiliwa na polisi, wakati wawili wanaendelea
kusakwa ikiwa ni pamoja na mjenzi ambaye kapewa masaa 12 kujisalimisha.
Kuna habari kwamba jengo hilo refu kulia pia linajengwa na mkararasi
aliyejenga hili lililoporomoka na kila aliye sehemu hii analiangalia kwa
jicho la wasiwasi
Rais Kikwete akiwa eneo la
tukio tena leo, baada ya kutembelea jana, akitoa maagizo kwa Kamanda wa
Kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova kwamba kila aliyehusika na
ujenzi wa jengo hilo kuanzia mchoraji, msimamizi na mjenzi wahojiwe na
wawajibishwe wakipatikana na kosa
Rais Kikwete akiongea na viongozi wa msikiti wa Shia ithnaasheri wakati anaondoka eneo la tukio
Eneo la tukio ambapo jengo
la ghorofa zaidi ya 10 liliporomoka jana asubuhi na hadi kufikia saa
sita mchana leo maiti 18 zilikuwa zimeopolewa na watu wanne wakiwemo
wakandarasi waliokuwa wanajenga pamoja na wahandisi wa halmashauri ya
wilaya ya Ilala wanashikiliwa na polisi, wakati wawili wanaendelea
kusakwa ikiwa ni pamoja na mjenzi ambaye kapewa masaa 12 kujisalimisha.
Kuna habari kwamba jengo hilo refu kulia pia linajengwa na mkararasi
aliyejenga hili lililoporomoka na kila aliye sehemu hii analiangalia kwa
jicho la wasiwasi.Picha na IKULU
Comments