Meneja wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina
Nkurlu(kulia)akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani)juu ya Promosheni ya MAHELA wakati wa kuchezesha droo ya
kuwapata washindi wa shilingi milioni moja moja ambapo washindi tisa
walipatikana hivi leo,kupitia promosheni hiyo,wanaoshuhudia kutoka
kushoto ni Ofisa wa Bodi ya Kubahatisha nchini Bw.Humudi Hussein na
Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael.
Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin
Michael(katikati)pamoja na Meneja wa Mahusiano wa kampuni hiyo,Bw.
Matina Nkurlu, wakimpigia mmoja wa washindi wa promosheni ya Mahela
aliejishindia shilingi Milioni moja, kushoto ni ofisa wa Bodi ya
Kubahatisha nchini Bw.Humudi Hussein, bado shilingi Milioni 251
zinaendelea kushindaniwa katika promosheni hiyo.
Ofisa wa Bodi ya Kubahatisha nchini Bw.Humudi Hussein kushoto
akiandika jina la mmoja wa washindi waliojinyakulia shilingi milioni
mojamoja kati ya washindi tisa kupitia promosheni ya MAHELA
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,katikati ni Meneja wa huduma za ziada
wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael,pamoja na Meneja wa Mahusiano wa
kampuni hiyo,Bw. Matina Nkurlu.
No comments:
Post a Comment