Monday, March 25, 2013

KAJALA AHUKUMIWA MIAKA 5 AU FAINI MIL 13, WEMA AJIANDAA KUMLIPIA


Msanii Kajala Masanja

HUKUMU ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar.
Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 213. Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Taarifa tulizozipata ni kwamba msanii Wema Sepetu anajiandaa kupeleka faini ya shilingi milioni 13 ili kumnusuru na kifungo msanii mwenzake. Taarifa zaidi tutazidi kuwajulisha.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...