Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni na
mmoja wa wageni waalikwa wakikagua magari mapya aina ya Volkswagon ya
Kampuni ya Alliance Autos kwenye showroom mpya iliyozinduliwa jana
jijini Dar na Waziri wa Uchukuzi Dr. Mwakyembe.
Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia
ya Ujerumani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika
hafla ya uzinduzi wa Showroom mpya ya magari ya Volkswagon ya Kampuni
ya Alliance Autos iliyopo Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa CFAO Motors Mama Maria Petro
akipokea wageni waalikwa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uchukuzi Mh. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na
wageni waalikwa pamoja na ujumbe wa wafanya biashara kutoka Ujerumani
walioongozwa Balozi wa Ujerumani nchini Klaus –Peter Brandes katika
hafla ya kuzindua Showroom ya magari ya kampuni ya Alliance Autos
inayouza magari aina ya Volkswagon ambapo pamoja na mambo mengine
amepongeza hatua hiyo na kusema serikali iko bega kwa bega na wafanya
biashara wabunifu na pia kuuhakikishia ujumbe kutoka Ujerumani kuwa
serikali imeweka mazingira bora ya kuwekeza hivyo wasisite kujitokeza.
Mkurugenzi
wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp(kulia) wakifurahia hotuba ya Dkt.
Mwakyembe.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp akizungumza
wakati wa uzinduzi huo ambapo amesema kufuatia kupanuka kwa kampuni ya
Alliance Autos na kuongezeka kwa wateja tumeonelea ni vizuri kufungua
showroom mpya ya magari ya Volkswagon ambapo wateja wanaweza kuitembelea
wakati wowote.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia)
akifurahia jambo wakati Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy
Sharp (hayupo pichani) akisoma hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa
Showroom mpya ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos
(T) LTD. Kulia ni Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya
Uchumi na Teknolojia wa Ujerumani. Kushoto ni Tender Manager wa CFAO
Motors Bw. Marco Kahabi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa
Ujerumani, Prof. Harald Braun (wa pili kushoto).
Warembo
wa Volkswagon waliokuwa wakikaribisha wageni kwenye hafla ya uzinduzi
wa showroom mpya ya Kampuni ya Alliance Autos iliyopo maeneo ya
Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed (kulia) akibadilishana mawazo na mmoja wa wateja waliohudhuria uzinduzi huo.
Picha
juu na chini ni Wakwetu Band ikiongozwa na Carola Kinasha kutoa
burudani kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa showroom mpya na ya
kisasa ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos.
No comments:
Post a Comment