Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Sadifa Hamis Juma akihutubia
aktika mkutano wa UVCCM uliofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa shule ya
msingi Mkwajuni, Kata ya Kichangani mkoani Morogoro leo Machi 3, 2013,
ikiwa ni mwisho wa ziara yake na viongozi wa kitaifa wa Jumuia hiyo
mkoani humo, kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na UVCCM
Mbunge
wa Morogoro, Abdulazizi Mohammed Abood akieleza utekelezaji wa ilani ya
CCM, baada ya kupandishwa jukwaani na Sadifa (wapili kushoto) wakati wa
mkutano huo.
Sadifa akikabidhi kadi ya Umoja wa CCM, kwa mwanachama mpya wakati wa mkutano huo. Jumla ya wanachama 1700 walipewa kadi.
Sadifa
na baadhi ya viongozi wakishirikina na wanachama kula kiapo cha CCM
baada ya wanachama wapya wa UVCCM kupewa kadi kwenye mkutano huo
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela akihutubia kwenye mkutano huo
Mmoja wa vijana machachari aliyehama hivi karibuni kutoka Chadema, Mtela Mwampamba akihutubia kwenye mkutano huo.
"Vijana
Chadema wanawazingua tu, wanawahamasisha kufanya maandamano ili
wawapige picha za kwenda kuonyesha nchi za nje kwa mafariki zao kwa
ajili ya kupatiwa mamilioni ya fedha", anasema Mwampamba kwenye mkutano
huo. Kulia ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya UVCCM Kaka Mpokwa.
VIjana wakiwa wamembeba Mwampamba baada ya kuingiwa na hotuba yake kwenye mkutano huo
Kama
Mwampamba, Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema
(BAVICHA) Taifa, Juliana Shonza, ambaye amehamia CCM hivi karibuni,
akibebwa na vijana wa UVCCM, baada ya 'kuimwagia razi' Chadema jukwaani
kwenye mkutano huo.
"Hawa
walijaribu kuwapiga mawe ili msifike kwenye mkutano huu, lakini tazama
mlivyofurika! Sasa ninasema, Uwezo wa kuwapiga tunao na nia ya kuwapiga
tunayo..Tutawapiga, lakini sisi hatutawapiga kwa mawe ila kwa sera zetu
makini" akasema Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda wakati
akihutubia kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Morogoro, Abdulaziz Mohamed Abood akiongoza msafara wa pikipiki kwenda kwenye mkutano huo
Vijana wakiserebuka kwa nyimbo za hamasa kwenye mkutano huo
"Raaaaaaa UVCCM" Vijana hawa wa CCM wakati wa shamrashamra kwenye mkutano huo
Kujimwaya mwaya hakukukoma hadi mwisho wa mkutano.Picha zote zimeletwa hapa na Bashir Nkromo-idara ya itikadi na uenezi CCM
No comments:
Post a Comment