Tanzania yataka isaidiwe kukusanya takwimu

00er 76bc2
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dr. Albina Chuwa ambaye anaongoza ujumbe wa  Tanzania katika Mkutano wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa,  Mkutano huo  unajadili  taarifa mbalimbali zinazohusiana na masuala ya takwimu. Tanzania ni Mjumbe wa Kamisheni hiyo.   Akichangia  majadiliano kuhusu taarifa ya mpango wa  uboreshaji na ukusanyaji wa takwimu za uhalifu,
Dr. Chuwa amesema,  nchini zinazoendelea Tanzania ikiwa moja wapo  zinahitaji  uwezeshwaji katika eneo hilo hasa ikizingatiwa kwamba uhalifu  baina ya nchi moja na  nyingine unatofautiana na kwa sababu hiyo hata ukusanyaji na uandaaji wa taarifa na takwimu zake hauwezi kufanana kutoka na utofauti wa kimazingira na uhalisia wa nchi husika na kusisitiza kwamba mpango wowote kuhusu  eneo hilo lazima uzingatie mahitaji ya nchi. Aliyekaa nyuma ya   Dr.   Chuwa ni  Mkurugenzi  wa   Shughuli za Takwimu, Bi. Redegunda Maro.
00er1 33201
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi (2012) Hajjat Amina Mrisho Said akifuatilia majadiliano   kuhusu masuala mbali mbali  yahusuyo Takwimu katika Mkutano wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.

Na Mwandishi Maalum
Tanzania imeshauri kwamba nchi zinazoendelea zisaidiwe katika ukusanyaji, uchambuzi na
utayarishaji wa takwimu zinazohusu masuala ya uhalifu.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,(NBS) Dr.
Albina Chuwa, wakati alipokuwa akichangia taarifa kuhusu mpango Makati kuhusu wa
uimarisha wa ubora na upatikanaji wa takwimu zinazohusu makosa ya jinai katika katika
ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.
Taarifa hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Takwimu na Geografia ya nchini Mexico kwa
kushirikiana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Madawa na Uhalifu.
Dr. Chuwa anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu
ya Umoja wa Mataifa.Mkutano huo unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
ukiwakutanisha wataalam wa masuala ya Takwimu kutoka nchi mbalimbali.
Katika mchango wake, licha ya kuwashukuru waandaji wa taarifa hiyo, Mkuu huyo wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu amesema, ni vigumu kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania kuutekeleza
mpango huo kutokana na upana wake na vile vile kutozingatia uhalisia na mahitaji ya kila
nchi.
Dr.. Chuwa, kama ilivyo kuwa kwa wachangiaji wengine akabainisha kuwa hata aina
ya makoja ya jinai yanatofautiana
kati ya nchi nchi na kwa sababu hiyo hata namna ya
ukusanyaji wa taarifa zake unapashwa kuzingatia mahitaji ya kila nchi.
“ Makosa ya jinai yanayotokea kwa mfano Tanzania hayawezi kulinganishwa au kufanana na
yale yanayotokea nchini Marekani, kwa hiyo hata ukusanyaji wa taarifa zake, pia utatofautiana
kwa kuzingatia aina ya makoa ya jinai na mapana yake” akasisitiza na kuongeza.
Lakini “ jambo la msingi zaidi, ni kwamba kwa nchi kama Tanzania tuna hitaji kuwezeshwa
ili ukusanyaji wa takwimu zinazohusu jinai, maandalizi yake na uainishaji wake uweze kuwa na
ubora na viwango vya kimataifa.
Baadhi ya wajumbe wengine waliochangia ajenda hiyo, walikwenda mbali zaidi kwa kutaka
kuainishwa au kuwepo na tafsiri sahihi kuhusu jinai u, badala ya kuuweka makosa yote ya jinai
katika kundi moja.
Aidha wajumbe wengine walitaka pia kuwapo kwa mafunzo, vipaumbele, uratibu na uwiano
katika suala zima la ukusanyaji wa takwimu zinazohusu jinai .
Mkutano huo wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, licha ya kujadili taarifa
ya mpango mkakati wa kuimarisha ubora na upatikanaji wa takwimu za jinai , pia umejadili
taarifa za takwimu nyingine nyingi zikiwamo zinazohusu masuala ya elimu, jinsia, mazingira,
biashara, ajira, huduma, uchumi, viashiria vya maendeleo , sayansi na teknolojia, kilimo,
sekta isiyo rasmi, takwimu zinazohusu bei, na takwimu zinazo husu afya.

Comments