Mkuu
wa Kitengo cha Usalama, CHADEMA, Wilfred Rwakatare, akionyesha
vidole viwili huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi wakati alipofikishwa
kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana nyuma yake ambae nae
amenyosha vidole viwili juu ni Joseph Ludovic Rwezaura wote kwa pamoja
wamefunguliwa Mashtaka
Mkuu wa Kitengo cha Usalama, CHADEMA, Wilfred Rwakatare, akionyesha
vidole viwili akiwa na Joseph Ludovic Rwezaura(Mwenye Flana ya Mistari) wote kwa pamoja wamefunguliwa Mashtaka
Sehemu ya Wafuasi wa Chadema Walifika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Willfred Lwakatare (wapili
kulia) na Ludovick Rwezahura (kulia) wakiondolewa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu na askari kuelekea kupanda gari kwa ajili ya
kurudishwa rumande, Dar es Salaam, jana.
Mbunge
wa Singida Magharibi-Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani
Bungeni Tundu Lissu(Kulia)akijadiliana Jambo na Mbunge wa Arusha
Mjini_Chadema Godless Lema (Mwenye Shati Jeupe Kati)Nyuma Mwenye Shati
la Mistari ni Vicent Nyerere Mbunge wa Chadema Musoma Mjini.Picha na
Chadema na Mdau Michaeal Jamson
----
Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru, Wakili wa Serikali Mkuu, Prudence Rweyongeza kuwa washtakiwa hao walifanya kosa la kula njama na kutenda makosa ya jinai kinyume na kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Rweyongeza alidai kuwa Desemba 28, mwaka jana katika eneo la King’ong’o katika wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama kwa kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru Msacky, kinyume na kifungu cha 227 cha sheria ya kanuni ya adhabu.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea........>>>>>
----
Dar es Salaam. Mkuu wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Ludovick Rwezaura
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu waki kabiliwa na
mashtaka manne likiwamo la kula njama ya kutenda kosa la jinai la kutoa
sumu kwa nia ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis
Msacky.
Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru, Wakili wa Serikali Mkuu, Prudence Rweyongeza kuwa washtakiwa hao walifanya kosa la kula njama na kutenda makosa ya jinai kinyume na kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Rweyongeza alidai kuwa Desemba 28, mwaka jana katika eneo la King’ong’o katika wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama kwa kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru Msacky, kinyume na kifungu cha 227 cha sheria ya kanuni ya adhabu.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea........>>>>>
No comments:
Post a Comment