Raisi
wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Erasto G. Chipungahelo akimkaribisha
Mratibu wa masoko wa Chuo kikuu cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya
Umma.
Mratibu wa Masoko wa Chuo kikuu cha waandishi wa Habari Bi Sophia akiwakaribisha washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 Chuoni hapo.
Mratibu wa Masoko wa Chuo kikuu cha Waandishi wa Habari na
Mawasiliano Bi Sophia Akizungumza Jambo na Washiriki wa Miss Utalii
Tanzania 2012/13 .
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 wakiwa wanajiandaa
kusikiliza mambo kadhaa kutoka kwa Mratibu wa Masoko Bi Sophia.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 wakiwa katika picha
ya Pamoja na Mratibu wa Masoko wa Chuo Kikuu cha waandishi wa habari na
Mawasiliano.
--
Chuo
Kikuu cha Waandishi wa kimewapongeza Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13
kwa elimu walizo nazo na kuwasihi watumie elimu zao kutangaza utalii wa
Tanzania Jambo ambalo lina manufaa makubwa kwa jamii ya Watanzania
Akizungumza na washiriki hao Kijitonyama Jijini Dar es salaam,
Mratibu wa masoko wa chuo hicho ndugu
Sophia Ndibalema aliwataka kutumia Fulsa ya kuwa warembo hasa utalii
kwa kujitaftia nafasi zaidi za elimu ya juu kwa manufaa yao Jamii na
Taifa kwa ujumla, alisema nafasi zipo wazi kwa wale wenye kuhitaji na
wenye sifa za kujiunga chuoni hapo kwa nafasi ya Cheti, Diploma na
Shahada, alisema amefurahishwa na muonekano wa asili na mavazi ya
heshima kwa washiriki hao hivyo kuondoa dhana kuwa washiriki wa urembo
kuwa ni wale wanaovaa mavazi yenye Kudhalilisha jamii hii inathibitisha
kuwa Miss Utalii ni Zaidi ya Mashindano Mengine na ni Alama ya Urithi
wa Taifa na kielelezo cha mwanamke au Binti wa Kitanzania
Comments