Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema akiongea katika
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na benki
hiyo Dar es Salaam juzi. Mkuu huyo alikuwa mgeni rasmi.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakisikiliza
hotuba na kupiga makofi kwa kuvutiwa na hotuba ya mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Jumla wa Professional Approach Group Modesta
Mahiga akitoa ushuhuda wa mafanikio kama mwanamke.
Mwenyekiti wa Ecobank Tanzania, Rukia Shamte
(mweye ushungi) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema. Kulia
ni Mkurugenzi Mtendaji Enoch-Osei Safo na Mkurugenzi wa Jumla wa Professional
Approach Group Modesta Mahiga.
Baadhi ya wafanyakazi wanawake ambao ni viongozi
katika benki hiyo wakitambulishwa kwa wageni.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali wa Ecobank
Fredrick Kanga akiongea wakati wa hafla.
*** ***
Ecobank Tanzania ambayo ni mojawapo
ya benki katika kundi la Ecobank Afrika, leo inaadhimisha siku ya wanawake
duniani katika sherehe iliyoandaliwa na benki hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa
Mhe. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
Sherehe hii ilifanyika kwa heshima
ya wadau wote wanawake kutoka Ecobank na sekta ya benki nchini. Katika
kuadhimisha mandhari ya siku hii “kupata kasi” Ecobank iko katika mstari wa
mbele katika kuongeza kasi katika kukuza ushirikishwaji wa fedha kwa wanawake
ambao wanalo jukumu muhimu sana katika kukuza uchumi wa Tanzania.
Bw. Enoch Osei-Safo Mkurugenzi wa
Ecobank alisema, ‘tunatambua nafasi ya wanawake katika jamii yetu. Wanawake
ndio kundi kubwa la wazalishaji wa chakula nchini, wafanyabiashara ndogondogo
na za kati. Vilevile, wao ndio wanaotoa asilimia kubwa zaidi ya mapato yao
katika kukuza familia na jamii. Wanawake wamechangia mno katika utoaji wa elimu
kwa watoto na mahitaji ya msingi kwa jamii na hapo ili kuwawezasha zaidi,
tulizindua upya akaunti ya watoto Pambazuka
amabayo inawapa wazazi uwezo wa kuwawezasha
wanao kusoma.’
Ecobank ina nia ya kuwawezesha watu na biashara Afrika ili kuwapa uwezo wa
kupata mafanikio kutokana na rasilimali tulizo nazo hapa Afrika
Meneja mwajiri wa Ecobank Tanzania Bi.
Maryam Mgeni alihakiki ahadi ya Ecobank
katika kukuza nafasi ya wanawake katika jamii kwa kutambua thamani yao katika
sehemu za kazi, na mchango wao wa kipekee nchini.
‘ Benki yetu imefaidika kutokana na
ujuzi na maarifa ya wafanyakazi wetu wa kike. Kutoka kwa ngazi ya mwenyekiti wa
bodi, wanawake wamechangia kwa kiasi kikubwa
katika ukuaji wa benki yetu.’
Comments