Monday, March 18, 2013

WANACHAMA SIMBA WAUONDOA UONGOZI WA RAGE MADARAKANI

Mzee wa Simba, Ally Mselemu akizungumza wakati wa mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Mkutano wa dharura wa klabu ya Simba, Mohamed Wande akifafanua jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Starlight jijini Dar es Salaam jana na kumg’oa madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutanohuo, Bi. Chuma Suleiman ‘Hindu’ na Katibu wa Mkutano huo, Mohamrd said.
 Mwanachama wa Simba Saidi Mkumba cheche.
Mwanachama wa Simba, sofia lubuva akitoa nondo zake za kumtaka Rage kung'oka madarakani.Picha Zote na Mdau Dande Francis

--
ZAIDI ya wanachama 700 wa klabu ya Simba Jana wameung'oa madarakani uongozi wa klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake Ismail Rage, huku majukumu wakimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope.

Wanachama hao walifikia maamuzi hayo, katika mkutano huo wa dharura uliofanyika ukumbi wa Starlight jijini Dar es Salaam, baada ya wajumbe walioudhuria kupiga kura juu ya kuwa na mashaka na uongozi uliopo madarakani.

Mara baada ya kupiga kura hizo wanachama hao walipendekeza Hanspope kwa kushirikiana na Al Kharoos ‘Malikia wa Nyuki’ katika kamati ya muda ambayo itafanya kazi yake mpaka msimu huu 2012/2013 utakapomalizika.

Mkutano huo, ulioongozwa kwa amani na utulivu chini ya Mwenyekiti wake Mohamed Wande, ulitoa fursa kwa wanachama kutoa maoni yao kabla ya kutoa maamuzi hayo kwa mujibu wa ibara ya 16(g) inayowaruhusu wanachama kuunda kamati ya muda ambayo itaisimamia Simba mpaka uchaguzi mkuu utakapofanyika mara baada ya kutokuwa na imani na viongozi.

Baadhi ya wanachama waliotoa maoni walipendekeza Rage abwage manyanga popote alipo na kudai kuwa anaendesha timu kidikteta na kisiasa huku wakimshinikiza kuendelea na siasa ili awaachie Simba yao, wao wenye mapenzi nayo.

Wanachama hao, Amina Mkumba kadi namba (05226) alisema “Rage hatufai Simba, kwa udanganyifu ambao ameufanya katika klabu yetu mpaka tunafungwa ni zamu yake na yeye kufungwa sasa tumechoka, usajili wenyewe danganya toto tumemchoka,”alisema, Nae Salm Simba (05864) alisema “Alisema wanachama tunatakiwa kuungana na kuwa kitu kimoja, na hapa tumopendekeze kamati ambayo itachunguza matumizi ya pesa za Simba na tukibaini udanganyifu Rage alipe,”alibainisha.

Mbali na hao nae Mzee Abdallah Jahali kadi namba (58) alisema “Rage huko aliko ajing’oe mwenyewe maana tumemchoka kila siku propaganda tu mara uwanja mara Okwi hata fedha zake hatuzioni anatufanya watoto tumechoka jamani nadhani hata picha la Yondani na Twite mnalikumbuka,”alisema.

Huku Ras Simba (5757) alilitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na Chama cha Usajili hapa nchini kulitazama suala hili kwa jicho la tatu na kudai kuwa viongozi wao hawafuati katiba hata kidogo ambayo imetungwa kwa ajili ya kuiongoza Simba

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...