WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete,amemteua Prof. CUTHBERT F. MHILU, Mhadhiri wa Chuo Kikuucha Dar
Es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania,
TBSkuanzia tarehe 18 Februari, 2013.
Kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Omary Kigoda (Mb), ameteua Wajumbekumi na moja wa Bodi hiyo. Wajumbe walioteuliwa na mahali wanapotoka ni kamaifuatavyo.
Kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Omary Kigoda (Mb), ameteua Wajumbekumi na moja wa Bodi hiyo. Wajumbe walioteuliwa na mahali wanapotoka ni kamaifuatavyo.
S/N | JINA | TAASISI ANAKOTOKA |
01. | Bw. Geofrey Simbeye | Mwakilishi wa TPSF |
02. | Bi. Fatma Riami Diwani | Mwakilishi wa Viwanda Vidogo na Vya kati |
03. | Bw. Michael Kamba | Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali |
04. | Dkt. Pamela L. Sawa | Mwakilishi wa Wizara ya Afya |
05. | Bi. Magdallena Utouh | Mwakilishi wa Tume ya Ushindani |
06. | Bw. Jasson B.B Bagonza | Mwakilishi wa Wizara ya Fedha |
07. | Bw. Juma Rajabu | Mwakilishi wa Umoja wa wajumbe wenye uelewa wa masuala ya Viwango |
08. | Bw. Rashid A. Salum | Mwakilishi wa Umoja wa wajumbe wenye uelewa wa masuala ya Viwango, Zanzibar |
09. | Prof. Ntegua Mdoe | Mwakilishi Vyuo vya Elimu ya Juu |
10. | Dkt. Fidea L. Mgina | Mwakilishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara |
11. | Bw. Leandry Kinabo | Kaimu Mkurugenzi Mkuu |
Uteuzi wa wajumbe hawa, unaanza mara moja.
Imetolewa na Wizaraya Viwanda na Biashara
S.L.P 9503
DARES SALAAM.
S.L.P 9503
DARES SALAAM.
No comments:
Post a Comment