Mkongwe
wa Muziki wa Kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo almaarufu, Lady Jaydee usiku wa
kumkia leo alifanya uzinduzi wa video yake mpya aliyomshirikishja Mkongwe
Mwezake katika burudani hiyo, Joseph Haule ‘Prof. J’ Video ya Wimbo unaokwenda
kwa jina la ‘JOTO HASIRA’.
Jaydee
alifanya uzinduzi huo katika mgahawa wake wa Nyumbani Longe uliopo Namanga
wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mamia ya wapenzi wa
Burudani na muziki wa mwana dada huyo.
Uzinduzi
huo ulisindikizwa na bendi ya Lady Jaydee ya Machozi Band na kutoa burudani
ambayo ilikonga nyoyo za mashabiki wake.
Pichani
juu ni Lady Jaydee akiimba wimbo wake huo mpya wa Joto Hasira kwaheri shida,
mbele ya mashabiki wake wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo huo.
Jaydee akiwa kando ya gari lake mara
baada ya kuwasili Nyumbani Lounge tayari kwaajili ya uzinduzi wa Video yake
mpya ya Joto Hasira.
Lady JayDee akitoa burudani mbele ya
mashabiki wake
Lady
JayDee akifanyiwa mhojiano na vyombo mbalimbali vya habari zikiwepo
Televisheni, magazeti, Redio na Blogs, ambazo zilituma wawakilishi wao katika
uzinfduzi huo.
Ben Paul nae alikuwepo Nyumbani Longe kushuhudia uzinduzi huo wa JOTO HASIRA hapa akishow love na washkaji
Prof.J
ameshiriki katika wimbo huo wa Lad JayDee Joto Hasira nae alikuwepo
Ukumbini hapo, hapa akipiga picha na Warembo walio pamba show hiyo.
Wadau mbalimbali walikuwepo kutoka pande mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.
Nyumbani Longe ilijaa vilivyo watu mbalimbali kuanzia walio na majina hadi akina wewe na mimi.
No comments:
Post a Comment