Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Kenya
yanaonyesha kuwa Uhuru Kenyatta, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee
Jomo Kenyatta anaongoza, huku akifuatiwa kwa karibu na aliyekuwa Waziri
Mkuu wa nchi hiyo, Raila Odinga.
Kama alivyo Uhuru,
Raila pia ni mtoto wa mmoja wa waasisi wa taifa la Kenya, ambaye alikuwa
Makamu wa Mzee Kenyatta, Jaramong Oginga Odinga.
Hadi
majira haya ya saa 12.17 alfajiri ya leo, Uhuru ambaye ni mgombea
wa TNA alikuwa amepata kura 1,617,701 sawa na asilimia 54.79 wakati Raila
ambaye ni mgombea wa ODM alikuwa akifuatia kwa kupata kura 1,201,910 sawa
na asilimia 40.68.
Matokeo hayo ni kutoka katika vituo
zaidi ya 8,300 kati ya 31,000 na yalikuwa yakionyeshwa moja kwa moja na
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) kadri yalivyokuwa
yanaingia.
Hata hivyo Mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan
akizungumza na vyombo vya habari jana usiku alisema matokeo hayo ni ya
awali na kwamba matokeo kamili yangetangazwa na tume yake baada ya
kukusanya taarifa kutoka vituo vyote vya kupigia kura.
Wagombea
wengine walikuwa wameachwa mbali. Hao ni Musalia Mudavadi, Peter
Kenneth, James Kiyiapi, Martha Karua, Mohamed Dida na Paul Muite.
Thousands of Nairobi residents lose sleep in effort to beat long queues
BOFYA MATOKEO KENYA KUONA MATOKEO HAYO LIVE
No comments:
Post a Comment