Monday, March 18, 2013

Lowasa asaidia kukusanya Sh85 mil za ajira kwa vijana

  •  Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa akisalimiana na vijana wa Boda Boda wa Arusha Mjini wakati alipokutana nao hivi karibuni
    photo5 5a214
    Na: Happy Lazaro- Arusha
    Waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amefanikisha kukusanywa kwa Sh85 milioni katika harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana, mkoani Arusha. Harambee hiyo iliyofanyika juzi, iliandaliwa na Umoja wa Waendesha Pikipiki (Uwapa) wa Jiji la Arusha. Akizungumza katika harambee hiyo, Lowasa ambaye pia
ni Mbunge wa Monduli, aliwataka vijana kujiepusha na ushawishi wa wanasiasa wanaowarubuni ili kushiriki katika maandamano yasiyokuwa na tija.
Badala yake, aliwataka wajikite katika kuzungumzia maendeleo yao. Alisema fedha zilizopatikana katika tukio hilo, ni vyema zikatumika katika kukopeshana ili kupanua mitaji ya biashara zao.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...