Monday, January 20, 2025

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA






Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora. 

Akizungumza Januari 20, 2025 katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji Bajeti ya vyuo vya Ardhi Tabora (ARITA) na Morogoro (ARIMO) ya mwaka 2024/2025, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Timotheo Mzava  amesema, uamuzi wa Wizara kutenga fedha ni mzuri na muhimu katika maendeleo ya vyuo hivyo na wanafunzi kwa ujumla.

"Msisitizo wa kamati yetu, vyuo hivi vya ardhi ni taasisi muhimu ya kuandaa wataalamu sambamba na kusaidia kazi, hivyo Wizara ya Ardhi iendelee kutupia jicho kwenye vyuo hivi ili vienedelee kufanya kazi yao inavyopaswa" amesema Mhe. Mzava.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa za vyuo hivyo kwenye Kamati, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi aamesema Wizara yake imepokea maelekezo ya kamati kwa utekelezaji na ufanisi wa vyuo hivyo.

Kikao hicho cha Kamati ya Bunge kimehudhuriwa Viongozi wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga, Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemela, Wajumbe wa Menejimenti ya wizara pamoja na watendaji wa vyuo vya ARITA na ARIMO.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...