Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe akiagana na Prof. Braun.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akiwa katika mazungumzo na
Prof. Harald Braun, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani
alipomtembelea Wizarani na kuzungumzia masuala mbalimbali ya kuimarisha
ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani.
Mhe. Membe akifurahia jambo kwa pamoja na Prof. Braun na Balozi Brandes mara baada ya mazungumzo yao.
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo
na Prof. Braun huku wajumbe waliofuatana na Katibu Mkuu huyo wa
Ujerumani akiwemo Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Mhe. Claus Peter
Brandes (mwenye tai nyekundu kushoto) na wajumbe kutoka Wizarani
akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Dora Msechu (wa
kwanza kushoto kwa Waziri) wakisikiliza.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
No comments:
Post a Comment