Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua kutoka uongozi wa
Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa
wanachama wake na kufanyika jana ukumbi wa Starlight, Dar es Salaam.
Vilevile
katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa
wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu
wa katiba ya klabu hiyo.
Kutokana
na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria,
Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa
kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.
Hata
hivyo, TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama
wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na
kanuni zilizopo. HABARI NA FATHER KIDEVU http://mrokim.blogspot.com/2013/03/tff-yapokea-barua-toka-uongozi-halali-wa.html
No comments:
Post a Comment