Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd azindua rasmi safari za ndege za kitalii moja kwa moja kutoka Afrika Kusini hadi Zanzibar
Rubani
wa Ndege ya Shirika la Mango Airlines Kepteni Kevin Viljoen akizungumza
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kutua
kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar kuanza safari za kuleta abiria kati
ya Afrika Kusini na Zanzibar. Nyuma ya Kepteni Kevin ni Kaimu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Juma Dunia Haji.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimaliza kuzindua safari za ndege za
shirika la Mango Airlines kati ya Afrika Kusini na Zanzibar katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar uliopo Kisauni. Kulia yake ni
Kaimu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Juma Duni Haji
na Kushoto yake ni Mwakilishi wa Shirika la Mango Airlines hapa Zanzibar
Bw. Javed Jaffery.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisoma hotuba ya
uzinduzi rasmi wa safari za watalii kutoka moja kwa moja Afrtika kusini
hadi Zanzibar kwa usafiri wa shirika la Mango Airlines katika uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Kisauni Nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Baadhi
ya Watalii 175 waliotua uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa kutumia ndege
ya shirika la Mango Airlines wakifurahia ukarimu wa kinywaji cha dafu
mara tu baada ya kutua uwanjani hapo. Picha na Hassan Issa-Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
--
--
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema asilimia 80%
ya mapato ya fedha za kigeni zinazoingia Nchini kupitia Sekta ya Utalii
inaweza kubakia kuwa ndoto kama suala la amani na utulivu
halitazingatiwa na kupewa nafasi yake chini ya usimamizi wa Jamii kwa
mashirikiano na Serikali Kuu.
Amesema
hakutakuwa na mgeni wala Mtalii atakayekuwa na shauku ya kutaka kuingia
Nchini sambamba na kufifia biashara ya Utalii endapo amani na utulivu
uliopo utachezewa na hatimae kutoweka kabisa.
Balozi
Seif Ali Iddi ameeleza hayo wakati akizindua rasmi safari za ndege za
shirika liitwalo Mango Airlines kati ya Afrika Kusini na Zanzibar,
kufuatia ushawishi uliofanywa na Kampuni ya utembezaji watalii Zanzibar
ya Gallery Tours, hafla iliyofanyika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Zanzibar uliopo Kisauni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Amesema
Taasisi, Jumuiya na hata watu wanaohudumia wageni na watalii wanapaswa
kuendeleza zaidi ukarimu uliopo Nchini ambao ni miongoni mwa utamaduni
unaoikuza Zanzibar Kiutalii katika Mataifa ya Nje.
“
Hakika vivutio tulivyokuwa navyo mfano Utamaduni, fukwe, bustani za
ndani ya Bahari, Mambo ya kale, wanyama adimu ni mali kubwa, lakini mali
zaidi katika vyote hivyo ni amani na utulivu”. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Serikali kwa upande wake
itajitahidi kutunza na kuidumisha amani na wale wanaotishia usalama wa
wananchi na mali zao watachukuliwa hatua zinazostahiki kwa mujibu wa
sheria bila ya kumuonea mtu.
Ameipongeza
Kampuni ya Gallery Tours kwa uratibu wake uliofanikisha Kampuni ya
Mango Airlines kuanzisha safari zake kati ya Afrika ya Kusini na
Zanzibar na kuyataka Makampuni mengine popote pale yalipo kuanzisha
safari kama hizo baina ya mataifa mbali mbali duniani na Zanzibar.
Balozi
Seif ameyahakikishia makampuni yatakayotumia fursa hiyo kuwa Serikali
itayapatia mashirikiano ya hali ya juu lengo likiwa ni kurahisisha
uingiaji wa watalii ili kuimarisha sekta hiyo muhimu kwa sasa.
Amefahamisha
kwamba safari za ndege zitakazofanywa na Kampuni ya Mango Airlines
kati ya Afrika Kusini na Zanzibar ni miongoni mwa kishawishi
kitakachoongeza idadi ya watalii wanaotoka Nchini humo kutembelea
Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema soko hilo la Afrika Kusini ni
kubwa na ni lazima kwa makampuni yanayohusika na sekta hiyo kujiimarisha
ili kupata watalii wengi zaidi.
“
Mwaka 2012 idadi ya watalii kutoka Afrika Kusini ni kubwa na ilifikia
watalii elfu 11,145 na kuchukuwa nafasi ya Tano miongoni mwa Nchi
zilizoleta watalii wengi hapa Zanzibar”. Amefafanua Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iiddi aliipongeza Wizara ya
Habari, Utamaduni ,Utalii na Michezo Zanzibar kwa juhudi zake
zilizopelekea kufanikisha harakati hizi za kukuza utalii nchini.
Akimkaribisha
mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Kaimu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo Mh. Juma Duni Haji alisema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar inathamini moyo na juhudi za Makampuni hayo kwa uamuzi wao wa
kuekeza katika sekta ya Utalii ambayo ni sehemu ya muhimili wa Uchumi wa
Taifa.
Mh.
Juma Duni alifahamisha kwamba Serikali inaelewa kwamba vipo vivutio
vingi vya ushawishi wa Utalii katika Mataifa mbali mbali Duniani lakini
kampuni hizo zikaonelea kufanya biashara zao Zanzibar.
Kaminu
Waziri huyo wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo alieleza kuwa
muelekeo wa utoaji wa huduma za Utalii zitaongeza kiwango cha mchango
wa fedha za kigeni kupitia Sekta hiyo.
Mapema
Mwakilishi wa Kampuni ya Mango Airlines hapa Zanzibar Bw. Javed Jaffery
alisema safari za ndege za Kampuni hiyo kati ya Afrika Kusini na
Zanzibar zilianza Disemba mwaka uliopita lakini zikasitishwa kutokana na
upungufu wa abiria kati ya pande hizo mbili.
Bw.
Jaffery alieleza kwamba kuanza tena kwa safari hizo kumekuja kutokana
na ongezeko la idadi ya makampuni yanayoshughulikia sekta ya Utalii
kushawishi abiria kutumia kituo cha Zanzibar kama kiunganishi kwa safari
zao katika Mataifa mengine Duniani.
Jumla
ya abiria mia moja na Sabini na Tano wameteremka kutoka ndani ya ndege
hiyo ya Mango Airlines ikitokea moja kwa moja Afrika Kusini chini ya
usimamizi wa Rubani wa Ndege hiyo Kepteni Kevin Viljoen na wana anga
wenzake.
Comments