Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakikata utepe
kuzindua rasmi hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya
Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert
Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, Machi 16, 2013
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert
Kairuki, Mama Koku Kairuki akimkabidhi tuzo Rais Jakaya Mrisho Kikwete
kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya nchini
wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo Machi 16, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu
Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika
sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo
Machi 16, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za
miaka 25 ya hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es
salaam, Machi 16, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi,
Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim wakiangalia watoto wachanga
waliotunzwa katika chumba maalum muda
mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu
mbalimbali za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa
mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake Machi
16, 2013.
Msanii Mrisho Mpoto akiburudisha wakati wa sherehe za miaka
25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, Machi
16, 2013
Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria sherehe za miaka 25
ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, Machi 16,
2013
Sehemu ya wageni waalikwa na wanafunzi na wafanyakazi wa
hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25
ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, Machi 16,
2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Waziri
Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, na viongozi wa hospitali ya Hubert
Kairuki wakiwa katika picha ya pamoja na vijana waliozaliwa katika hospitali hiyo miaka 25 iliyopita Machi 16, 2013.Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment