Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo huku ujumbe kutoka Japan ukimsikiliza.
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.),
akizungumza na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Japan,
Bw.Osamu
Fujimura alipofika na ujumbe wake Ofisini kwa Mhe. Waziri leo ambapo
walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na
Japan ikiwemo maandalizi ya Mkutano wa Tano unaohusu Ushirikiano kati ya
Japan na Afrika (TICAD V) utakaofanyika nchini humo mwezi Juni 2013.
Mhe. Membe akimsikiliza Bw. Fujimura wakati wa mazungumzo yao.
Mhe. Masaki Okada (kulia), Balozi wa
Tanzania hapa nchini akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati
ujumbe kutoka Japan ulipomtembelea Mhe. Membe ofisini kwake. Wengine
katika picha ni Balozi Mbelwa Kairuki (katikati), Mkurugenzi wa Idara ya
Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
na Bw. Khatib Makenga, Afisa katika Idara hiyo.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya
pamoja na Bw. na Bibi Fujimura (kushoto) na Mhe. Masaki Okada (kulia),
Balozi wa Japan hapa nchini mara baada ya mazungumzo.Picha Zote na Tagie Daisy Mwakawago-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
No comments:
Post a Comment