Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (kushot) akimkaribisha
Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania Balozi Japhet Issack
alipomtembelea ofisini kwake leo.Pamoja na mambo mengine Balozi huyo
amemuomba Spika Makinda kuimarisha uhusiano na Bunge la Namibia kwani
kuna mambo mengi Bunge hilo linaweza kujifunza kutoka Tanzania.
Spika
Makinda akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Balozi wa Namibia
nchini Tanzania ambapo amemhakikishia Balozi huyo kuwa Bunge la Tanzania
lipo tayari kushirikiana na Bunge la Namibia na kuona ni maeneo yapi
ambayo yatawafaidisha wananchi wa nchi mbili hizi. Aliainisha maeneo ya
mafunzo na kujenga uwezo kuwa ya kipaumbele.Picha Na Prosper Minja-Bunge.
No comments:
Post a Comment