**********************************************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Leo tarehe 13 Februari
2013, Shirika la Nyumba la Taifa linapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa
lipo katika mchakato wa kuboresha mazingira upangaji na upangishaji na leo
linataka kutoa taarifa kuu mbili muhimu.
1. Kupangishana katika nyumba za
Shirika bila Kibali (Illegal Subletting)
Mwaka 2010, Shirika liliwatangazia watu
waliopangishwa kwenye nyumba za Shirika kinyume cha taratibu wajitokeze ili
waweze kupewa upangaji moja kwa moja na Shirika. Baadhi yao walijitokeza na
walipewa upangaji.
Hata hivyo imeonekana kuna ambao hawakujitokeza
kwasababu yoyote ile, Shirika sasa linawatangazia tena wajitokeze ili waweze
kuhalalishwa ukaaji wao (kupewa upangaji wa Shirika). Wanaombwa kujitokeza
ndani ya kipindi cha miezi mitatu (kuanzia tarehe ya taarifa hii).
Baada ya hapo fursa ya kutambuliwa haitakuwapo
tena, bali watatolewa kwenye nyumba hizo na zitapangishwa kwa watu wengine.
2.
Uhuishaji wa mikataba ya upangaji (Lease Renewal)
Mwaka 2006 Shirika lilifanya uhakiki wa
wapangaji pamoja na kutoa mikataba mipya yenye muda maalumu baada ya kufuta ile
iliyokuwa haina kikomo. Imeonekana kuna wapangaji ambao hawakujitokeza kipindi
hicho, wengine waliopewa mikataba ya
muda maalumu imeshakwisha muda wake.
Shirika limefanya juhudi mbalimbali ikiwamo
kuwaandikia barua za kuwakumbusha kwenda ofisi za Shirika kuchukua mikataba,
baadhi wamekwenda na wengine hawajafanya hivyo na kubaki bila mikataba.
Shirika linapenda ifahamike kuwa kwa mpangaji
kutokuwa na mkataba kwasababu yoyote ile ina maana kwamba hajakubaliana na
masharti ya upangaji. Shirika linatoa muda wa mwezi mmoja kuanzia tarehe ya
taarifa hii kwa yeyote ambaye mkataba wake umemaliza muda au hana mkataba afike
ofisi za Shirika ili aweze kupewa mkataba.
Shirika linapenda kusisitiza kuwa kutokufanya
hivyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja
uliotolewa tachukuliwa kuwa ni ukiukaji wa masharti ya upangaji na baada ya
hapo wale wote ambao watakuwa hawana mikataba ya upangaji . Shirika
litalazimika kuwatoa kwenye nyumba kwani watakuwa wameonyesha kuwa hawahitaji
upangaji.
Shirika pia linapenda ifahamike kuwa halina
mikataba ambayo haina kikomo wala mikataba ya mwezi kwa mwezi. Pia mkataba ili
ukamilike lazima uwe umesainiwa na pande zote mbili yaani Shirika la Nyumba na
mpangaji anayetambulika.
IMETOLEWA
NA:
KITENGO
CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
SHIRIKA
LA NYUMBA LA TAIFA
3 comments:
I've been browsing online more than three hours as of late, but I by no means discovered any fascinating article like yours. It is pretty price enough for me. In my view, if all site owners and bloggers made good content material as you probably did, the net might be a lot more useful than ever before.
my page :: gadgetshop.com voucher codes
My page > information technology for the health professions
Ηi, I lоg on to your blog on a regular basiѕ.
Your humoristіc style iѕ witty, κeeр doing what уou're doing!
Review my web site :: internet marketing for dummies
Aρpreciating the persistence you ρut into уour wеbsіte and detaіled
infοrmatiоn you present. It's great to come across a blog every once in a while that isn't the
ѕаme outԁated rеhаshed infoгmаtiοn.
Fantastiс rеaԁ! I've bookmarked your site and I'm
аdding youг RЅS feedѕ to my Gοogle account.
My webpаge: computershare.co.uk/careers
Post a Comment