Kesi ya Uchozi na Uharibu wa mali inayo
mkabili Sheikh Ponda Issa Ponda leo imeendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Jijini Dar es Salaam huku Polisi wakiwa katika doria kali ya kuimarisha
ulinzi katika viunga jirani na Mahakama hiyo ambayo imejizolea umaarufu mkubwa
jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kwa jinsi inavyo endesha kesi na
watu wa aina mbalimbali kufikishwa katika mahakma hiyo kabla ya baade kesi zao
kuhamia Mahakama Kuu kwa hatua zaidi za kisheria.
Father Kidevu Blog ilikuwepo kufuatilia
matukio ya hapa na pale na zifuatazo ni picha mbali mbali za tukio hilo na pia
kesi hiyo inataraji kuendelea tena Mahakamani hapo kesho.
Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa katika basi la Magereza tayari kwa kurejeshwa Mahabusu.
Msafara ukianza kutoka Mahakama ya Kisutu
Wafuasi waliokuwa nje wakiimba wakati gari likitoka
Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa Pondawakilifuatilia gari lililombeba kiongozi wao wakati akitoka Mahakama ya Kisutu.
Mkazi
wa jiji akipita kando ya kundi la Askari nje ya Mahakama ya Hakimu Mkzi
Kisutu wakati Askari hao walipo imarisha Ulinzi nbje ya Mahakama hiyo.
Ustaadh huyu alitishiwa na Mbwa akataka kutoka baruti
Wengine zaidi wakitoka Mahakama ya Kisutu
Wakiwapokea na kuwapongeza wenzao wanao tuhumiwa pamoja na Ponda
Kundi la Wafuasi likiwa limejikusanya karibu na Jengo la Sophia House huku Polisi wakiwa kando yao.
Doria barabarani nayo ilikamilika
Ulinzi ulikuwa ni wa Uhakika
Mbwa maalum wa Polisi nao walikuwa kazini hapa wakikata kiu kutokana na jua kali.
Hapa ni Fanya Fujo Uone kilicho mfanya Kanga akose Manyoya shingoni. Picha zote za Mroki Mroki ukitaka kupata tukio zima kwa kina angalia Mroki mroki
No comments:
Post a Comment