Baadhi ya wafuasi wa Shekh Ponda wakiwa wamekamatwa kwa tuhuma za kufanya maadamano bila kibali cha polisi.
Wafuasi hao wa Shekh Ponda wakipandishwa kwenye gari la polisi mara baada ya kukamatwa katika maandamano hayo.
Zoezi la kuwakamata na kuwapeleka polisi watuhumiwa hao likiendelea chini ya ulinzi mkali.
Ulinzi ulikuwa ni mkali sana. Polisi wa Pikipiki wakiwa kazini Jana
Magari mbalimbali yakiwa yamebeba askari Polisi yakipita mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam Jana.Picha na John Bukuku
---
Katika tukio hilo Uhuru FM imeshuhudia Maduka mbalimbali yakiwa
yamefungwa katika Mitaa ya Kariakoo kutokana na maandamano hayo ya watu
wanaodaiwa kuwa Waumini wa Dini ya Kiislam.
Licha ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuzuia
maandamano ya Waumini wa Dini ya Kiislam, baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni
Waumini wa Dini hiyo katika maeneo ya Buguruni, Malapa na Kariakoo wamefanya
maandamano hayo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi kupitia Vikosi vya Kutulia
Ghasia-FFU-limelazimika kutumia Mabomu ya Machozi ili kuwatawanya waandamanaji
hao waliokuwa wamebeba Mabango na Mawe kwenye Mifuko katika Mitaa ya Malapa
pamoja na Kariakoo.
Waumini hao wanashinikiza Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa
Mashitaka-DPP-kumwachia kwa dhamana Katibu wa Jumuiya ya Waislam Shekh PONDA
ISA PONDA ambaye anakabiliwa na kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu.
Jana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar e s salaam kupitia kwa Kaimu Kamanda wake AHMED MSANGI lilipiga marufuku kufanyika kwa mandamano hayo kutokana na kutokuwa na kibali cha Polisi.
No comments:
Post a Comment