Mwenyekiti
wa CCM ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu mwenyekiti wa CCM Bara
Ndugu Philip Mangula (kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman
Kinana wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa White House uliopo katika
makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo.Rais Kikwete amefungua na kuongoza
semina kwaajili ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa ambayo pamoja
na mambo mengine itachagua wajume wa Kamati kuu.
Baadhi
ya wajumbe wa kamati kuu ya CCM taifa wakihudhuria semina maalum
iliyofunguliwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete katika ukumbi wa White House,Makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akielekeza jambo wakati wa
ufunguzi wa Semina maalum kwaajili ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM
taifa iliyofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa White House makao makuu
leo.Kushoto anayesikiliza kwa makini ni Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa
CCM bara Pius Msekwa.Wengine katika picha ni Rais Wa Zanzibar ambaye pia
ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein(Wapili
kushoto),Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana(wanne kushoto), na
kulia ni Makamu Mwenyekiti CCm Bara Ndugu Philip Mangula(Picha na Freddy
Maro)
No comments:
Post a Comment