Rais Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la utoaji vitambulisho vya taifa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
leo amezindua rasmi zoezi la utoaji vitambulisho vya taifa katika
sherehe zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali wakiwemo
marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Amani Abeid
Karume. Baada ya zoezi la uzinduzi, Rais Kikwete aliwakabidhi baadhi ya
viongozi vitambulisho vyao vya taifa.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi alisema ni muhimu
kuwa na vitambulisho vya Taifa kwani ni jambo la msingi ambalo litaweza
kuwa na manufaa makubwa kwa kuunganisha mifumo mikubwa ya usajili ya
kitaifa.
Baadhi
ya mifumo hiyo ni kama Mfumo wa usajili wa kodi(TRA), Mfumo wa vizazi
na vifo(RITA),Mfumo wa pasi za kusafiria(UHAMIAJI),Mfumo wa POLISI,
Mifumo ya mawasiliano ya simu(Vodacom,Tigo,Zantel, Airtel,TTCL),Mfumo
wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara Serikalini, Mifumo ya Hifadhi za
kijamii,Mifumo ya Taasisi za kifedha,Mifumo ya udahili ya Wanafunzi(Loan
Board),n.k.
Mkurugezi
Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu alizitaja changamoto mbalimbali za
kiutendaji zikiwemo wananchi kukosa viambatanisho muhimu vya
kuwatambulisha,uhakiki wa taarifa za uraia,Uhakiki wa taarifa za
makazi,Upungufu wa vifaa na Rasilimali watu.
Aliyataja mahitaji halisi ya zoezi
hilo kuwa ni vifaa vya kuchukulia alama za vidole, picha saini
takribani 12,000, rasilimali watu wa muda 114,000 na wakudumu 3000 ili
kukukamilisha mpango huo kwa muda utaotakiwa.
No comments:
Post a Comment