Picha Juu Mamia ya wakazi wa Dar es salaam walijitokeza kuunga mkono maandamano
yaliyoandaliwa na chadema kupinga Uonevu wanaofanyiwa wabunge wa
Upinzani Bungeni.
Viongozi wa chadema wakiwa katika mshikamano mkubwa, wakiandamana
kupinga vitendo vya uonevu vinavyofanywa na Spika na Naibu wake dhidi ya
wabunge wa Upinzani.
Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akiwa jukwaani katika mkutano wa
kulaani vitendo vya uonevu kwa wapinzani. Mkutano uliofanyika katika
kiwanja cha mwembeyanga Temeke leo.
Mbunge
wa singida Magharibi-Chadema na Mnadhimu mkuu wa kambi ya Upinzani
Bungeni, Tundu Lissu akiongea kwenye mkutano uliofanyika Viwanja vya
Mwembeyanga
Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema,John Mnyika akiongea katika mkutano.
Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema, Godbless Lema naye akimwaga cheche jukwaani.
Mbunge wa iringa Mjini-Chadema, Pter Msigwa akiunguruma
Mbunge wa Kawe-Chadema,Halima Mdee amesema tukianza 2014 itakula kwetu, tuanze sasa.
Katibu mkuu wa AFP amesema chama chao kinaunga mkono chama makini kama Chadema
Viongozi wa Chadema wakiwa Meza kuu kutoka kushoto katibu mkuu Dr
Wilbroad Slaa, Mwenyekiti Mh Freeman Mbowe na naibu katibu mkuu Mh Zitto
Kabwe.Picha Zote na CHADEMA
----
VIONGOZI na mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana walifanya maandamano na kuhitimishwa kwa mkutano wa hadhara uliofanyika Temeke, jijini Dar es Salaam ambako chama hicho kilitangaza nia ya kuandaa hoja ya kuwang’oa viongozi wa Bunge.
----
VIONGOZI na mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana walifanya maandamano na kuhitimishwa kwa mkutano wa hadhara uliofanyika Temeke, jijini Dar es Salaam ambako chama hicho kilitangaza nia ya kuandaa hoja ya kuwang’oa viongozi wa Bunge.
Hoja hiyo itawasilishwa katika mkutano ujao wa
Bunge kwa ajili ya kuwapigia kura za kutokuwa na imani na Spika wa
Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai kwa madai ya kukwamisha
mijadala yenye masilahi ya wananchi bungeni.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Uwanja wa Temeke Mwisho, Dar es Salaam, wabunge wa chama hicho
wakiwa na uongozi wa juu, waliwataka wananchi waliohudhuria mkutano huo
kujiandaa na maandamano ya kuwang’oa spika hao.Kana kwamba hiyo
haitoshi, wabunge hao walitangaza namba za simu za viongozi hao wa Bunge
ili wananchi wazitumie kuwashinikiza wang’oke.
Akihutubia katika mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu
wa chama hicho (Bara), Zitto Kabwe alisema Spika Makinda ameshindwa
kuwajibika na hivyo anapaswa kung’olewa kutokana na kutaka kuirudisha
nchi kwenye kipindi cha kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu
(Epa).
Akizungumzia kitendo cha Spika Makinda kuifuta
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto aliyekuwa
Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema imefutwa kwa mbinu za CCM kuzima sauti
ya wabunge wa upinzani wanaozungumzia masilahi ya wananchi.Kwa habari zaidi bofya na Endelea.....>>>>
No comments:
Post a Comment