Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akimkabidhi bajaji mpya mlemavu wa miguu ambaye ni mfanyakazi wa
TANROADS Bi.Sarah Nalingigwa Nkumbo huko ikulu mjini Dodoma(picha na
Freddy Maro)
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumapili, Februari
10, 2013 amekabidhi pikipiki aina ya bajaj kwa mama mmoja mlemavu, Mama Sarah
Mkumbo Nalingigwa katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu Ndogo mjini Dodoma.
Mama Nalingigwa ni
mtumishi wa Wakala wa Barabara nchini – TANROADS- katika Mkoa wa Singida na
shughuli ya leo imehudhuriwa pia na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa John Pombe
Magufuli, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mufugale na Mama Salma
Kikwete.
Shughuli ya makabidhiano
ya leo, inatimiza ahadi ambayo Mheshimiwa Rais aliitoa kwa Mama Nalingigwa
wakati alipokutana naye miongoni mwa wananchi waliohudhuria sherehe ya utiaji
jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi=Chaya mjini Itigi, Mkoa
wa Singida Novemba mwaka jana.
Akizungumza mara baada
ya kukabidhi pikipiki hiyo, Rais Kikwete amemwambia mama huyo: “Nimefurahi
kwamba nimeweza kutimiza ahadi yangu. Hii ndiyo faraja yangu kwamba sasa
utaweza kufanya kazi zako kwa urahisi zaidi, utaweza kutembea kwa urahisi zaidi
na kufika kazini na kurejea nyumbani kwa namna ya haraka zaidi.”
Naye Mama Nalingigwa
amemwambia Rais Kikwete: “Wewe ni kiongozi shupavu, kiongozi hodari na
mpiganaji anayemjali kila mtu. Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu akujalia ili
uendelee kuwaona wengine wenye mahitaji kama ya kwangu.”
Ameongeza mama huyo
ambaye amefanya kazi Wizara ya Ujenzi kwa miaka 30 iliyopita: “Kwa kuniwezesha
kiasi hiki, umenipa uwezo wa kufanya kazi kwa namna bora zaidi., Ni vyema kuwa
viongozi wengine wakaiga mfano wako wa kujali watu walioko chini yako.”
No comments:
Post a Comment