Tuesday, February 19, 2013

MELI YA KIVITA YA KIRUSI YA KUPAMBANA NA UHARAMIA MARSHAL SHAPOSHNIKOV’ YAWASILI DAR

Balozi wa Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akipokea salamu kutoka kwa kiongozi mkuu Rear Admiral Vladimir Vdovenko wakati alipotembelea meli hiyo bandarini.

Meli ya kivita  ya kupambana na uharamia aina ya  Anti Submarine iitwayo  Marshal Shaposhnikov’,  ilipokuwa ikiingia na kasha baadae kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, kwa ziara fupi yenye lengo la kuimarisha urafiki baina ya Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na Urusi. 
Wakati nchi ya Somalia ikiendelea kuwa kitovu cha uharamia, jumuiya ya kimataifa ilikubaliana kudhamiria kupambana na vitendo hivyo viovu. Lakini hadi sasa, wakati nchi nyingine zikitumia mbinu mbalimbali katika mapambano hayo, ni nchi za Russia, India na China pekee zinazosindikiza meli zao za biashara na nyinginezo ili kuzilinda na uharamia.
Meli hiyo imewasili siku ya Jumamosi na inategemea kuondoka kesho, Jumatano.
 Wanajeshi wa Kirusi wakionesha umahili wao wa ukakamavu muda mfupi kabla Balozi wan chi yao Mheshimiwa Rannikh hajapita mbele yao.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...