Jengo la Kisasa la Palace Hotel ambalo limefunguliwa leo na Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Naibu waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyarandu, alitoa wito huo jana wakati wa uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Palace Hoteli, ambayo imejengwa kwa ubia na Shirika la nyumba nchini(NHC).
Lazaro alisema uwekezaji huo utasadia kuongeza idadi kubwa ya watalii na mapato,”mwaka jana tulipata watalii 800,000 ukilinganisha na nchi ya Rwanda na udogo wake ilipata wageni 600,000 tatizo kubwa la nchi yetu ni upungufu wa vyumba vya kulala wageni”alisema.
Alisema mkakati huo utaufanya mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii kuzidi kuongeza idadi ya vitanda vya kisasa kulala wageni ambapo kwa sasa ina vitanda 2,800 tu nyuma ya mkoa wa Dar es salaam wenye vitanda 3,800 na kuzidi mkoa wa Mwanza wenye vitanda 900 licha ya ukubwa wake.
“Tunaomba shirika la nyumba lijitanue hadi
maeneo hasa ujenzi wa hoteli za kisasa za kitalii…na sisi wizara tunahitaji
wawekezaji wa ndani na nje kujitokeza kujenga katika maeneo ya wazi na ndani ya
hifadhi zetu panapofaa…na tumejipanga kukabiliana na watumishi wenye urasimu
wanaokwamisha watu wenye nia njema”alisisitiza.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu
alisema ujenzi wa hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota nne, umegharimu kiasi
cha sh 16 bilioni ambapo NHC imetoa ardhi n ash 9 bilioni huku kiasi kingine
kikitolewa na Palace Hoteli.
Alisema mradi wa hoteli hiyo ni moja ya miradi ambayo imekuwa na manufaa makubwa, kutokana na uwazi katika uendeshwaji wake na hivyo kuingiza mapato kwa pande zote NHC na Mbia.
“binafsi nampongeza sana Mkurugenzi wa Palace hoteli, Dk Hans Macha kwa uwazi katika uendeshwaji wa mradi huu na tunamkaribisha katika miradi mingine aje tushirikiane”alisema Mchechu.
Naye Dk Ha Macha alisema mradi huo hadi sasa imetoa ajira ya wafanyakazi 120 na unatoa huduma nyingine kadhaa, ikiwepo huduma za kibenki na utachangia kwa kiasi kikubwa kikuza uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa.
“hoteli hii tunatumia malighafi za hapa Arusha toka kwa wajasiriamali ikiwa ni njia ya kuongeza ajira na kipato na pia tumekuwa na miradi mbali mbali ikiwepo na utunzwaji wa mazingira”alisema Macha.
Akifungua mradi huo rasmi, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipongeza mradi huo na kutoa wito kwa wajasiriamali wengine kujitokeza na kuingia ubia na NHC katika kutekeleza miradi mbali mbali.
Alisema mradi huo unakwenda vizuri na umeongeza mapato ya NHC kwani katika eneo hilo, kabla ya ujenzi wa hoteli walikuwa wakipata kwa mwaka kiasi cha sh 31 milioni pekee lakini sasa wanapata 151 milioni.
“natoa agizo rasmi kwa wabia wengine walioingia mikataba na NHC kama huu, kama hawajatekeleza hadi sasa basi mikataba yao ifutwe kwani ni hasara kwa shirika la Taifa”alisema Profesa Tibaijuka.
Jengo la Kisasa la Palace Hotel ambalo limefunguliwa leo na Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Hoteli Palace ilivyo kwa ndani
Na hapa ni hoteli hiyo ilivyo kwa nje
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akikata utepe wakati wa uzinduzi wa hoteli mpya yenye hadhi ya nyota nne ya Palace jijini Arusha jana.Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na kulia mmiliki wa hoteli hiyo Dk Hans Macha. Waziri wa Ardhi, Nyumba
Comments