Naibu
Katibu Mkuu wa Mali asili Dkt Bakari Assed akitoa ufafanuzi mbele ya
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kuhusiana
na athari zilizopatikana kutokana na kuungua kwa msitu wa Jozani.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia
uharibifu uliotokana na kuungua moto kwa msitu wa Jozani wakati
akitembelea aneo hilo
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na
wapiganaji wa kikosi cha zimamoto na uokozi angalia uharibifu uliotokana
na kuungua moto kwa msitu wa Jozani wakati akitembelea aneo hilo
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na
wapiganaji wa kikosi cha zimamoto na uokozi angalia uharibifu uliotokana
na kuungua moto kwa msitu wa Jozani wakati akitembelea aneo hilo. (Picha
na Salmin Said, OMKR)
Na Hassan Hamad OMKR
Zaidi
ya ekari 48 za msitu wa Hifadhi wa Jozani zimeungua moto kufuatia moto
uliozuka katika msitu huo siku nne zilizopita, na kusababisha hasara ya
zaidi ya shilingi bilioni tatu.
Akizungumza
wakati akitembelea eneo hilo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Maalim Seif Sharif Hamad amesema tukio hilo ni la kusikitisha na
limeitia hasara kubwa serikali na taifa kwa ujumla.
Amesema mbali na hasara hiyo ya kiuchumi lakini moto huo pia umesababisha athari kubwa za kimazingira ambazo zinaweza kuchukua muda mrefu kuweza kurudi katika hali yake ya kawaida.
“Inawezekana
baadhi ya wanyama adimu wamepotea, vyanzo vya maji vimeharibika na miti
adimu ya asili imeharibika, ukweli ni hasara kubwa”, alieleza kwa
masikitiko Maalim Seif.
Amewaagiza
maafisa wa msitu huo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha
kuwa hakuna watu wanaotumia njia za kizamani katika uvunaji wa asali ili
kuepuka athari zaidi zinazoweza kujitokeza.
Maalim
Seif amewataka wafugaji wa nyuki kufuata maelekezo ya wataalamu wa
Wizara ya kilimo na mali asili ili kufuata njia za kisasa za uvunaji wa
asali usiotumia moto ili kudhibiti uharibifu katika misitu ya asili.
“Misitu
yetu ya asili tunayoitegemea zaidi ni huu wa Jozani kwa Unguja na ule
wa Ngezi kwa Pemba, ni wajibu wetu tuilinde na tuihifadhi kwa nguvu zetu
zote ili isitoweke”,alisisitiza Makamu wa Kwanza wa Rais.
Nae
Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili Dkt. Bakari Assedi amesema chanzo cha
moto huo kinasadikiwa kuwa ni wavunaji wa asali wanaotumia njia za
zamani za kutumia moto.
Amesema msitu huo wa asili ambao pia ni hifadhi ya taifa, ni muhimu katika kulinda na kuhifadhi misitu na viumbe adimu ambapo kwa wastani kila baada ya miaka 15 kupatikana kiumbe kipya katika msitu huo.
No comments:
Post a Comment