TAARIFA KWA UMMA
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA NA TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD (TPL)
KUSITISHA ZOEZI LA KAMPENI
12/02/2013
1.
Kamati ya Uchaguzi, kwa mamlaka iliyonayo kupitia Kanuni za Uchaguzi za
TFF Ibara ya 3(1), 6(1) (g) na (l), 10(5), 11(6) inayosomeka pamoja na
Ibara ya 14(1) na (2) na pia Ibara ya 26(5) na (6), imesitisha zoezi la
kampeni za uchaguzi wa TFF na TPL Board lililokuwa lianze kesho tarehe
13/02/2013 hadi hapo itakapowatangazia, ili kuhakikisha kuwa mchakato wa
uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya
TFF.
2. Tarehe za Uchaguzi Mkuu wa TFF na TPL Board zinabaki kama zilivyopangwa.
3.
Taarifa hii inazingatia pia Ibara ya 2(4) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF
inayoagiza uongozi uliopo madarakani kuendelea na kutekeleza majukumu ya
Shirikisho hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.
Deogratias Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI TFF
No comments:
Post a Comment