Tuesday, February 12, 2013

Majina wa Wajumbe wa Kamati kuu ya CCM yatajwa

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha siku mbili Februari 10 na 11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi na kufanya uchaguzi wa wajumbe 14 wa Kamati Kuu yake.

Halmashauri Kuu ya Taifa ya imeridhia uteuzi wa Dk Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM.

Wajumbe 14 walioteuliwa kuwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu wa CCM ni :-

Wajumbe wa Kamati Kuu Bara
1. Stephen Masatu WASIRA
2.Pindi Hazara Chana
3.Professa Anna Kajumulo Tibaijuka
4. Jerry Slaa
5. Adam  Kimbisa
6. Dk Emmanuel Nchimbi
7. William Lukuvi

Wajumbe wa Kamati Kuu Zanzibar:
1. Ndugu Shamsi VuaiNahodha
2. Dk Hussein Mwinyi
3. Profesa Makame Mbalawa
4. Dr Salim Ahmed Salim
5. Dk Maua daftari
6. Hadija .H. Abuu
7. Samia Suluhu Hassan
Wamechaguliwa kwa kupigiwa kura na wajumbe wa NEC kutoka miongoni mwa majina 28 yaliyoteuliwa kugombea nafasi 14. Wapo saba kutoka Bara na saba kutoka Visiwani.



 












Wamechaguliwa kwa kupigiwa kura na wajumbe wa NEC kutoka miongoni mwa majina 28 yaliyoteuliwa kugombea nafasi 14. Wapo saba kutoka Bara na saba kutoka Visiwani.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...