Monday, February 25, 2013

AJALI MBAYA IRINGA GARI LARUKA HEWANI NA KUTUA JUU YA GARI JINGINE‏


Naibu meya  wa Manispaa ya Iringa Gravas Ndaki akishangaa ajali ya karne yenye maajabu makubwa kwa mkoa  wa Iringa  ,ajali  iliyotokea  usiku wa jana  eneo la Hoteli ya kati (makosa) au CRDB ya  zamani katika barabara ya Iringa -Dodoma, baada ya gari aina ya RAV 4 yenye namba T 319 AFL (juu) kuhama njia na  kuigonga  Taxi yenye namba  za usajili T 510 AYU yenye hakuna majeruhi  wala aliyepoteza maisha.

 
Ramadhani Mrisho maarufu kwa jina la Makosa  ambaye ana jina kubwa katika masikio…
 
Naibu meya  wa Manispaa ya Iringa Gravas Ndaki akishangaa ajali ya karne yenye maajabu makubwa kwa mkoa  wa Iringa  ,ajali  iliyotokea  usiku wa jana  eneo la Hoteli ya kati (makosa) au CRDB ya  zamani katika barabara ya Iringa -Dodoma, baada ya gari aina ya RAV 4 yenye namba T 319 AFL (juu) kuhama njia na  kuigonga  Taxi yenye namba  za usajili T 510 AYU yenye hakuna majeruhi  wala aliyepoteza maisha.
Ramadhani Mrisho maarufu kwa jina la Makosa  ambaye ana jina kubwa katika masikio ya  wakazi  wa mkoa  wa Iringa na Tanzania  kutokana na jinsi alivyokuwa maarufu  katika  mji  wa Iringa kwa  kumiliki mali mbalimbali na kutoa misaada kwa jamii ameibuka katika  eneo la ajali na kupinga ulevi kwa madereva.
 
Dereva  wa Taxi yenye namba T 510 AYU Bw Kelvin Kaduma akitengeneza gari yake baada ya kutolewa  eneo la ajali. (Picha Zote na Francis Godwin) 
Na Francis Godwin, Iringa
AJALI   mbaya  imetokea  mjini Iringa  eneo la Makosa ama CRDB ya  zamani kwenye barabara  kuu ya Iringa - Dodoma baada ya gari aina ya RAV 4 yenye namba T 319 AFL kuhama njia na  kuigonga  Taxi yenye namba  za usajili T 510 AYU iliyokuwa  ikiendeshwa na dereva Kelvin Kaduma.
Ajali  hiyo  imetokea majira ya saa 10 usiku wa  jana   wakati  dereva  wa RAV4 hiyo akitoka maeneo ya mji  wa Iringa akielekea  mwelekeo ambao wakazi  wa mji wa Iringa wamekuwa  wakipata  starehe zao eneo la  Dragon Bar na Club  Twistas  kuendelea  kumalizia starehe za mwisho  wa  wiki.
Mashuhuda  wa  tukio  hilo  wamemueleza mwandishi  wa habari hizi eneo la tukio kuwa  gari hiyo aina ya  RAV 4 ilikuwa katika mwendo mkali mfano  wa gari  lililopo katika mashindano na  hivyo dereva  wake  kushindwa kukata kona ya mnara  wa Manispaa ya Iringa  na hivyo  kugonga ukuta  wa  barabara hiyo  kabla ya  kuhama na kuigonga Taxi hiyo kwa  kuipanda  juu.
Hata  hivyo  mashuhuda hao  walisema  kuwa  dereva  huyo  wa RAV 4 alikuwa anaonekana  kulewa zaidi kutokana na mazingira  ambayo alikuwa akionekana kuwa ni mtu ambae amepata pombe kiasi.
Kwa upande  wake dereva  aliyegongwa na gari aina ya RAV 4 yenye namba T 319 AFL Bw Kelvin kaduma ambae  alikuwa akiendesha Taxi yenye namba  T 510 AYU alisema  kuwa alishuhudia  gari hilo RAV 4  likija kwa mwendo wa kasi na ndipo alipoamua  kusimama ili  kushuhudia na ghafla alijikuta akifunikwa na RAV 4 hiyo.
Alisema  kuwa  RAV 4 hiyo  iliruka  ukingo wa  barabara  ambao  una michongoma na kujengwa kwa  sementi na kutua  juu ya Taxi yake na kushindwa  kuendelea na  safari na kuwa  iwapo asingesimama kuona mtiti wa gari hilo basi dereva huyo wa RAV4 angekufa kwa  kugonga nyumba iliyopo jirani ambayo ina hoteli ya Hast Tast.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...