Tuesday, February 19, 2013

Lowassa akabidhi Bajaji nne maalum kwa kubebea mizigo zenye thamani ya shilingi millioni 50

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amekabidhi pikipiki nne za miguu mitatu maarufu kama Bajaji ambazo ni maalum kwa kubebea mizigo zenye thamani ya kiasi cha shilingi millioni 50,kwa umoja wa vijana wilaya ya Monduli ili kuwasaidia vijana waliokuwa wakikakabiliwa na tatizo la Ajira.Pichani ni Mh. Lowassa akikabidhi funguo za pikipiki hizo kwa mmoja wa viongozi wa matawi ya vijana wilayani hapo,ambao walifika nyumbani kwake Ngarash Monduli kwa ajili ya kupokea pikipiki hizo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...