TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: KUENGULIWA KWANGU KUGOMBEA URAIS WA TFF 2013
Ndugu
zangu,kupitia vyombo vyenu vya habari ninaomba niueleze umma wa
watanzania,hususani wadau wa mpira wa miguu,yafuatayo kuhusu kuenguliwa kwangu.
Awali
ya yote nieleze kusikitishwa kwangu na maamuzi yaliyotolewa na kamati ya rufaa
ya TFF ya kuniengua kugombea urais wa TFF.Sikubaliani na maamuzi haya .
Katika
kuniengua kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF imetoa sababu mbili (nanukuu
magazeti ya jana tarehe 12/02/2013 maana hadi leo sijakabidhiwa barua ya
kuenguliwa).
Kukosa
uadilifu kwa kupinga waraka uliotolewa
na TFF wa kubadili Katiba ya TFF mwezi Desemba 2012.
Kukosa
uzoefu wa miaka mitano ya uongozi.
Ndugu
zangu,kiini cha maamuzi ya Kamati ya rufaa dhidi yangu ni pingamizi lililowekwa
na mtu mmoja anayeitwa AGAPE FUE.Bwana Agape Fue aliniwekea pingamizi katika
kamati ya uchaguzi akidai mimi nilipinga
waraka wa kubadili katiba ya TFF na pia sina uzoefu wa miaka mitano ya uongozi
wa mpira.Kinyume na matakwa ya kamati ya uchaguzi kama yalivyotangazwa kuwa
mtoa pingamizi aje mwenyewe kutetea pingamizi lake ,Bwana Agape Fue hakutokea
mbele ya Kamati ya Bwana Lyatto.Matokeo yake tarehe 31/01/2012 kamati ya uchaguzi ya TFF ilitoa maamuzi ya ya kutupilia mbali
pingamizi hili.
Bwana Agape Fue hakuishia hapo kwa mara nyingine tarehe 06/02/2013 alikata
rufaa kwenye kamati ya rufaa ya uchaguzi akidai kamati ya uchaguzi haikumtendea
haki. Rufaa hii haikuwa na anwani wala namba ya simu ya Bw.Agape Fue.Rufaa ilisikilizwa tarehe
10/02/2013 na maamuzi ya kukata jina langu yakatangazwa jioni ya tarehe
11/02/2013.
Mpaka
leo najiuliza hivi huyu Bw. Agape Fue ni mwanaume au ni mwanamke?(hakueleza kama ni Bwana au Bibi
Agape Fue). Agape Fue ni nani hasa? Anaishi wapi?Je ni Mtanzania au sio
Mtanzania maana kikanuni wasio
watanzania hawaruhusiwi kujihusisha na uchaguzi wa TFF (rejea kifungu cha 9 cha
kanuni za uchaguzi),pingamizi lake halikuambatana na udhibitisha wa uraia. Kwa
nini alichukua maamuzi haya? Sipati jibu.
Iweje
mtu achukue maamuzi mazito ya kumkatia
mtu rufaa kisha uishie kusaini karatasi na kuwaachia wengine wakusemee na usije
hata kushuhudia kinachoendelea kama kweli una maslahi na madai yako? Waandishi
wa habari mnisaidie kupata majibu.
Ndugu
zangu ,mtoa pingamizi alidai haikuwa sahihi kupinga azimio la kubadili katiba
ya TFF kwa njia ya waraka.Naomba nisistize mambo matatu:
Wajumbe
wa mkutano mkuu wa TFF wanawakilisha matakwa ya vyama vilivyowatuma kwenda kwenye
mkutano mkuu wa TFF,na ndio maana
chama cha mpira cha mkoa wa Kagera (KRFA) kiliitisha kikao cha kamati ya
utendaji ili kamati iweze kutoa
mwongozo kwa wajumbe wake kuhusu nini
kifanyike kuhusu waraka ulioletwa na TFF,hivyo maamuzi yaliyotolewa ya kuukataa
waraka huu yalikuwa ni maamuzi ya chama cha mpira mkoa wa Kagera na wala
hayakuwa ni maamuzi ya Jamal Malinzi,iweje malinzi niadhibiwe kwa maamuzi
haya,kwa nini usiadhibiwe mkoa mzima na mikoa yote iliyopinga waraka?hii ni
haki kweli? Siamini kama kuna mjumbe wa mkutano mkuu aliyekiuka maamuzi ya
kamati yake ya utendaji.
Katika
mchakato wa kubadili katiba kwa njia ya waraka kilichokuwa kinagomba sio
maudhui (content) ya mabadiliko ya Katiba bali utaratibu uliotumika kubadili
Katiba. Swali la msingi tulilojiuliza wajumbe wa kamati ya utendaji KRFA ni kwamba je kwa mujibu wa Katiba ya TFF
kifungu 22 na kifungu 30 wapi katiba inatamka kuwa inaweza kubadilishwa kwa
njia ya waraka? Mpaka leo hilo jibu hakuna,labda aliyeniwekea pingamizi
atusaidie kupata jibu la swali hili. Katiba ya TFF iko wazi kabisa
inatamka kuwa Katiba itabadilishwa kwa
njia ya Mkutano Mkuu tu (General Assembly).
Ni
kweli FIFA iliagiza yafanyike mabadiliko ya Katiba ya kuingiza kipendele cha
‘club licencing’ katika Katiba ,lakini je FIFA katika agizo hilo ilisema Katiba
ya TFF ivunjwe ili kutimiza azma hiyo? Ikumbukwe kuwa mwaka 2004 FIFA iliagiza
TFF iingize kwenye Katiba kipengele cha Katibu Mkuu awe wa kuajiriwa badala ya
kuchaguliwa,agizo hili lilitekelezwa kwa kupitishwa na Mktano Mkuu wa TFF,iweje
leo utaratibu huu ukiukwe?
Hata
majuzi CAF walipotaka kubadili katiba ili Rais wa CAF atokane na wajumbe wa
Kamati ya Utendaji jambo hili lilitekelezwa kwa kuitisha mkutano mkuu wa
dharura uliofanyika Seychelles majuzi.
Katiba ndio msingi mkuu wa uendeshajiwa TFF,nitaipigania siku zote.Huo ndio
utaratibu,si CAF si FIFA si Vyama vya mpira vya nchi,hakuna anayebadili Katiba kwa njia ya waraka,kama kuna mwenye
ushahidi aulete.
Kuengua
jina langu eti kwa kuwa nilipinga waraka wa kubadili Katiba sio uamuzi sahihi.
Kuhusu
uzoefu wa miaka mitano katika Uongozi:
Ikumbukwe
kuwa katika uchaguzi mkuu wa TFF mwaka 2008 niligombea na jina langu lilikatwa
na kamati ya uchaguzi ya TFF.Nilikata
rufaa katika Kamati ya Rufaa ya TFF na kushinda . Hukumu hii ni halali hadi
leo.Iweje leo hii miaka minne baadae Kamati hiyo hiyo ya rufaa (kubadili majina
ya wajumbe sio kubadili taasisi) inione sina uzoefu?.Si hilo tu ,hata katika
kujaza fomu namba moja ya kugombea niliambatanisha vielelezo vyote vya uzoefu
wangu ikiwa ni pamoja na kudhibitisha kuwa katika kipindi cha miaka mine
iliyopita nimekuwa:
-Mjumbe
wa Baraza la michezo mkoa wa Dar es salaam.
-Mwenyekiti
wa kamati ya mashindano chama cha mpira mkoa wa Pwani COREFA.
-Mjumbe
wa mkutano mkuu wa mkoa wa Kagera
-Mwenyekiti
wa chama cha mpira mkoa wa Kagera
Hii
ni pamoja na kuongoza Yanga 2002-2005.
Hivi
katika nafasi hizi za uongozi ipi ni ya kuongoza ‘bonanza’? Nimedhalilishwa
sana.
HITIMISHO
Vyombo
vya habari kupitia makala,tahariri na maoni ya wasikilizaji/wasomaji/watazamaji
vimesifia sana awamu mbili za uongozi wa Bwana Leodeger Tenga.Bwana Tenga
amesifiwa kwa umahiri wake wa kuleta utulivu katika sekta ya mpira wa miguu
Tanzania.Amesifiwa kwa kujenga taasisi imara ambayo mhimili wake mkuu ni
sekretarieti makini na kamati mbali mbali zilizo imara .Let him rise to the
occasion,muda wa kuonyesha uongozi imara ni huu,historia itamhukumu kwa jinsi
gani atasimamia suala hili,haki sio lazima itendeke lakini pia inatakiwa
ionekane inatendeka.
Kamati
ya utendaji ya TFF inayo mamlaka ya kubatilisha maamuzi haya kwa maslahi ya
mpira wa Tanzania.Ninamshauri Rais wa TFF aitishe kikao cha dharura cha kamati
ya utendaji ili kijadili hali hii na kunirudishia haki yangu ya kugombea urais
wa TFF.
Nihitimishe
kwa kuwaomba wadau wa mpira wa miguu Tanzania
wawe watulivu wakati tukisubiri kupata ufumbuzi wa suala hili.
Mungu
ibariki Afrika,
Mungu
ibariki Tanzania.
Ahsanteni
sana,
JAMAL
MALINZI
S.L.P
10000 DAR ES SALAAM
13/FEBRUARY/2013
No comments:
Post a Comment