Thursday, February 07, 2013

Mkurugenzi Vodacom awatuza wafanyakazi bora

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza (kulia)akimkabidhi Abella Tarimo, Meneja biashara wa Vodacom Tanzania zawadi ya ngao na cheti kwa kuwa mfanyakazi bora katika kuunganisha idara zote kwa wakati na utendaji kazi kiufanisi. Anaeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wateja Harrieth Lwakatare.

Baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Masoko Vodacom Tanzania wakiwa wameshikilia hundi yao yenye thamani ya $ 5,000 mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Rene Meza (wa pili kulia)kwa kuibuka wafanyakazi bora kwa mwaka 2012/13.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza wa saba toka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kitengo cha Jasiliamali watu mara baada ya zawadi ya ngao na cheti wakati alipokuwa akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza,akiongea na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati alipokuwa akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo hayupo pichani akiongea nao wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...