Wednesday, July 29, 2015

WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA WANAWAKE NA WATOTO YA CENTENARY YA MJINI CANBERRA WAMEONYESHA NIA YA KUFANYA KAZI NCHINI TANZANIA

sa1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Caniberra nchini Australia inayotoa huduma ya Afya ya Mama, vijana  na watoto mara baada ya kufika eneo la hospitali kwa madhumuni ya kujionea namna bora yautoaji huduma.  Mama Salma yupo nchini Australia akifuatana na mumewe Rais Jakaya Kikwete kwenye ziara rasmi ya kiserikali nchni humo.
sa2
Mke wa Rais na Mama Salma Kikwete na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CaniberraMama Elizabeth Chatham wakibadilishana mawazo wakati walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ya mama, vijana na watoto.
sa4
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaangalia baadhi ya watoto wanapatiwa huduma ya matibabu katika hospitali ya Caniberra wakijishughulisha na michezo mbalimbali wakiwa na wazazi wao.
sa5
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpa pole na kumtakia apone haraka binti Addison Stephen,6, aliyevunjika mguu na kufungwa PoP na hatimaye kulazwa hospitalini hapo huku akihudumiwa na baba yake Mzazi Bwana Stephen Miles (aliyesimama kulia) na aliyechuchumaa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Mama Elizabeth Chatham.
sa6
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimbeba mtoto mchanga Isabella mwenye umri wa siku moja aliyezaliwa na uzito wa kilo 3 na gramu 8 katika hospitali ya Caniberra nchini Australia huku wazazi wake Bwana Steven Fanner,34, na Bibi Tania Mras,32, wakishuhudia tarehe 28.7.2015.
sa7
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake,WAMA, Mama Salma Kikwete akimkabidhi jarida linalochapishwa na Taasisi yake kwa Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi Matendaji wa Hospitali ya wanawake, vijana na watoto ya Caniberra nchini Australia mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbaali za kutolea huduma hospitalini hapo yarehe 28.7.2015.
sa8
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Gavana Jenerali wa Australia Mama  Cosgrove mara baada ya Rais Kikwete kukutana na Gavana Generali wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove kwenye Ikulu ya nchi hiyo tarehe 28.7.2015.
sa9
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ikulu ya Australia  huku Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyeji wake Gavana Jenerali Peter Cosgrove na Mkewe wakishuhudia.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
……………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu – Canberra, Australia 
 Wafanyakazi wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary ya  mjini Canberra wameonyesha nia ya kufanya kazi nchini Tanzania ili kumuunga mkono Mke wa Rais Mhe. Mama Salma Kikwete katika juhudi zake za kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia afya za wanawake, vijana na watoto wa Hospitali hiyo Liz Chatham wakati akiongea na Mhe. Mama Kikwete na ujumbe wake walipotembelea Hospitali hiyo.
Liz  alimshukuru Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kutembelea Hospitali hiyo na kujioneka kazi wanazozifanya pia alimpongeza kwa juhudi zake anazozifanya za kuhakikisha wanawake na watoto wa Tanzania wanapata huduma bora ya afya.
Mkurugenzi huyo alisema katika Hospitali hiyo wafanyakazi wengi  wa sekta ya afya wanapenda kwenda kufanya kazi Tanzania  ili waweze kutoa huduma ya afya kwa ajili ya mama na mtoto pamoja na watu wengine  na kubadilishana ujuzi wa kazi na wenzao.
Kwa upande wake Mhe. Mama Kikwete alisema  ni jambo la kufurahisha kuona katika Hospitali hiyo wanawake wenye afya njema wanajifungua katika mazingira mazuri na watoto ambao ni wagonjwa wanapewa matibabu na  uangalizi wa hali ya juu.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuwahudumia kinamama wajawazito na watoto, kujifungua iwe sababu ya kuwa na  furaha na kusherehekea lakini siyo tofauti na hapo, nasema hivi kutokana na mazingira halisi ya kule ninakotoka”.
Pamoja na kuwa jitihada za makusudi zinafanywa na Serikali bado wanawake na watoto wanapoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika”, alisema Mama Kikwete.
Akiwa katika Hospitali hiyo Mama Kikwete alipata nafasi ya kuongea na watoto ambao ni wagonjwa  ambao kwa wakati huo walikuwa darasani wanasoma na aliwaona  na kuwajulia hali wazazi waliojifungua Hospitalini hapo.
Utaratibu wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary mtoto akiwa amelazwa kipindi ambacho shule hazijafungwa anafundishwa masomo ambayo wenzake wanafundishwa darasani kwani Hospitalini hapo kuna madarasa na walimu wanaofundisha watoto wagonjwa.
Mama Kikwete ameambatana na mmewe Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Australia kwa ajili ya ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...