Thursday, July 16, 2015

MKURUGENZI MKUU MPYA TCRA AMTEMBELEA KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

1
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba(Kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo, Dkt.Ally Yahaya Simba ameteuliwa kushika nafasi ya Prof. John Nkoma aliyemaliza Muda wake.
2
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba(Kushoto) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga.
3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimueleza Dkt. Ally Yahaya Simba (Kushoto) umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya mawasiliano,alipomtembelea leo ofisini kwake.
4
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na kumhakikishia kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya Taifa hasa katika kuiendeleza Sekta ya Mawasiliano Nchini.
5
 Watendaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (mwenye suti nyekundu) alipotembelewa na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba (kulia kwa Katibu Mkuu) aliyeteuliwa kushika nafasi ya Prof. John Nkoma aliyemaliza Muda wake.
6
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Hawapo pichani), walipotembelewa na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba.Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Raphael Hokororo.
7
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiagana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba(kushoto)
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...