TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Vijana skauti 4 pamoja na kiongozi mmoja ni miongoni mwa washiriki wa Jamboree ya maskauti ya dunia itakayofanyika Nchini Japan katika mji wa Yamaguchi – Kihara hama kuanzia tarehe 28 Julai hadi 8 Agosti 2015.
Jamboree ya Skauti ya Dunia ni mkusanyiko wa Skauti kutoka nchi zote wanachama na kawaida hufanyika kila baada ya miaka minne kama iliv yo kwa mashindano ya mpira ya kombe la dunia.
Mwanzilishi wa Chama cha Skauti duniani Hayati Lord Baden Powell alianzisha mfumo wa Jamboree ya Skauti ya dunia kwa madhumuni ya kuwakutanisha vijana skauti kubadilishana mawazo na kujifunza mambo mbalimbali kutoka nchi tofauti tofauti.
Jamboree ya kwanza ya maskauti ya dunia ilifanyika London Uingereza mwaka 1920 na kuanzia mwaka huo imekuwa ikifanyika kila mwaka katika nchi tofauti tofauti.
Shirikisho la Vyama vya Skauti Dunia (WSB) World Scouts Bureau, ndio hupanga na kuchagua nchi itakayo andaa Kambi hili la kimataifa katika kipindi kijacho.
Chama cha Skauti Tanzania inapeleka idadi ndogo ya washiriki kutokana na gharama kubwa za ushiriki wa kambi hii. Jumla ya dola za kimarekani 4000 sawa na milioni 8 za Kitanzania ndio gharama za ushiriki kwa mshiriki mmoja.
Gharama hizo ni pamoja na usafiri, chakula malazi na ada ya ushiriki wa kambi hiyo ambayo huchukua karibu siku 10.
Shughuli zinazofanyika wakati wa Jamboree hiyo ni pamoja na mafunzo mbalimbali ya stadi za kiskauti, kazi za Jamii, Moto wa Kambi, na siku moja maalum ya Kimataifa ambapo kila nchi wanachama huandaa maonyesho maalum kuonyesha bidhaa mbalimbali walizonazo ikiwa ni pamoja na kuonyesha utamaduni wao.
Kikosi cha skauti kutoka Tanzania kinawakilishwa na
1. Eline Kitali – Kamishna Mtendaji na Mkuu wa Msafara.
2. Michael Malima kutoka mkoa wa D’salaam
3. James Mzoma Chinula kutoka mkoa wa Kilimanajaro
4. Malkia Ulimboka Mwakilili kutoka mkoa wa Mbeya
5. Martha Albert Bennie. Kutoka mkoa wa Mwanza.
Skauti hao wanatarajia kuondoka nchini Jumamosi tarehe 25 Julai 2015 na shirika la ndege la Emirates muda wa saa 10.45 alasiri na wanatarajia kurejea nchini 10 Agosti 2015.
No comments:
Post a Comment